Askari wa HMAS Melbourne wakiwa na madawa yaliyokamatwa.
Madawa hayo yakiharibiwa.
JESHI la
majini la Australia limekamata na kuharibu kilo 353 za madawa ya kulevya
aina ya heroin yenye thamani inayokadiriwa kuwa zaidi ya dola milioni
700 katika pwani ya Tanzania.
Askari wa
meli ya HMAS Melbourne waliyagundua madawa hayo katika meli moja
Jumatano iliyopita wakiwa katika shughuli za kupiga vita ugaidi na
kuimarisha usalama maeneo ya baharini Mashariki ya Kati na Bahari ya
Hindi.
Mkuu wa
kikosi hicho, Daryl Bates, alisema hatua hiyo ilikuwa ni pigo katika
kukwamisha njia za kupatikana kwa fedha zinazotumiwa na magaidi.
Credits: AFP
No comments:
Post a Comment