Katibu
Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Ndugu Job Masima kulia
akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya kukagua
gari aina ya Ashok Leyland iliyotolewa na Wizara yake kwa ajili
kuimarisha viteule vya kijeshi vya Kasanga na Kirando Mkoani Rukwa.
Katika kukabiliana na changamoto zilizokuwa zinavikabili vitua hivyo
Wizara ya ulinzi kupitia kwa Katibu Mkuu huyo imetoa gari mbili, boti
mbili na fedha Tsh. Milioni 150 kwa ajili ya kuboresha makazi na
miundombinu katika viteule hivyo. Kwa upande mwingine amesema kuwa
baadhi ya vifaa vingine vitatoka makao makuu ya jeshi katika kuboresha
viteule hivyo.
Katibu
Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Ndugu Job Masima kulia
akimkabidhi funguo ya gari Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya
kama ishara ya makabidhiano ya gari mbili pamoja na michango mingine
itakayotumika katika viteule vya jeshi vya Kasanga na Kirando Mkoani
Rukwa.
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akiwasha gari hilo kama ishara
ya kupokea misaada hiyo kwa viteule viwili vya Kirando na Kasanga
vilivyopo Mkoani Rukwa.
Katibu
Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Ndugu Job Masima wa
pili kushoto akitoa majumuisho ya ziara yake kwa uongozi wa Mkoa wa
Rukwa leo. Katika majumuisho yake pamoja na mambo mengine aliongeza kuwa
mchakato wa kupanua kiteule cha Kasanga utawekwa kwenye bajeti ya mwaka
ujao wa fedha ili kukiongezea ufanisi zaidi. Kwa upande wake Mkuu wa
Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya ambae ndiye chachu kubwa ya
mafanikio haya kwa kumualika Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi kuja
kujionea changamoto zilizopo amemshukuru kwa kuitikia wito wake na
mchango wa ujumla uliotolewa na Wizara yake katika kuimarisha ulinzi
katika ukanda wa ziwa Tanganyika unaopakana na nchi za Burundi, Zambia
na DRC.
Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Symthies Pangisa kushoto akizungumza
katika kikao hicho cha majumuisho ambapo amemshukuru Katibu Mkuu wa
Wizara ya Ulinzi na msafara wake kwa kazi nzuri waliyoifanya Mkoani
Rukwa katika kipindi chote cha ziara yake ya siku tatu.
Baadhi ya wajumbe walioshiriki kikao hicho cha majumuisho wakifuatilia kwa makini.
(Na Hamza Temba – Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa @Rukwareview.blogspot.com
No comments:
Post a Comment