Waziri
wa Elimu na Mafunzo ya Amali wa Zanzibar Mheshimiwa Ali Juma Shamhuna
mara alipowasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Muscat kuanza
Ziara ya kikazi nchini Oman, kushoto ni Waziri wa Elimu ya Juu wa Oman
Mhe. Dr. Rawiyah Al Busaidi, wa kwanza kulia ni Mheshimiwa Ali Ahmed
Saleh, Balozi wa Tanzania nchini Oman.
Waziri wa Elimu na
Mafunzo ya Amali wa Zanzibar Mheshimiwa Ali Juma Shamhuna wa pili kutoka
kushoto akiwa katika mazungumzo na Waziri wa Elimu ya Juu wa Oman Mhe.
Dr. Rawiyah Al Busaidi, wa pili kulia , wa kwanza kushoto ni Mheshimiwa
Ali Ahmed Saleh, Balozi wa Tanzania nchini Oman.
Waziri wa Elimu na
Mafunzo ya Amali wa Zanzibar Mheshimiwa Ali Juma Shamhunawa tatu kulia
akiongoza ujumbe wa Zanzibar katika mazungumzo na Waziri wa Elimu ya Juu
wa Oman Mhe. Dr. Rawiyah Al Busaidi akiongoza ujumbe wa Oman Kushoto ,
wa nne kushoto ni Mheshimiwa Ali Ahmed Saleh, Balozi wa Tanzania nchini
Oman.
Waziri wa Elimu na
Mafunzo ya Amali wa Zanzibar Mheshimiwa Ali Juma Shamhuna kushoto na
Waziri wa Elimu ya Juu wa Oman Mhe. Dr. Rawiyah Al Busaidi wakitia saini
nyongeza katika mkataba wa ushirikiano wa Elimu ya Juu baina ya Oman na
Zanzibar.
Waziri wa Elimu na
Mafunzo ya Amali wa Zanzibar Mheshimiwa Ali Juma Shamhuna kushoto akiwa
katika Mazungumzo na Waziri Kazi wa Oman kuhusu ushirikiano katika sekta
ya mafunzo ya amali.
Waziri wa Elimu na
Mafunzo ya Amali wa Zanzibar Mheshimiwa Ali Juma Shamhuna kushoto akiwa
na Mheshimiwa Ali Ahmed Saleh kulia , Balozi wa Tanzania nchini Oman
alipotembelea Ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini Oman pichani chini
maafisa wa ubalozi na ujumbe wa mheshimiwa waziri wakifuatilia
mazungumzo.
Waziri
wa Elimu na Mafunzo ya Amali wa serikali ya Zanzibar Mheshimiwa Ali
Juma Shamhuna, alifanya ziara ya Kikazi nchini Oman kuanzia tarehe 16
hadi 20 February 2014 kwa Mwaliko wa mwenyeji wake Mheshimiwa Dr.
Rawiyah Al Busaidi, Waziri wa Elimu ya Juu wa Oman.
Ziara hii ilikuwa na madhumuni makuu ya kuimarisha uhusiano wa
kindungu uliopo baina ya Oman na Tanzania kupitia sekta ya Elimu na
kuimarisha uhusiano wa karibu na ushirikiano baina ya taasisi za elimu
kati ya Tanzania na Oman.
Katika ziara hii Mhe. Ali Juma Shamhuna alikutana na kufanya
mazungumzo na Mwenyeji wake Dr. Rawiyah Al Busaidi ambapo pia walitia
saini nyongeza katika Mkataba wa Mashirikiano katika Elimu ya Juu baina
ya Zanzibar na Oman . Mheshimiwa Waziri Shamhuna pia alikutana na Waziri
wa Elimu wa Oman Mheshimiwa Dr. Madihana Ahmed Al Shibaniya na Waziri
wa Kazi wa Oman Mheshimiwa Abdullah Nassor Al Bakri, .
Mbali na kukutana na viongozi hawa wa Oman, Mheshimiwa Waziri
Shamhuna alipata nafasi kutembelea maeneo kadhaa kujonea shughuli
mbalimbali za Taasisi zinazoshughulika na elimu za Oman, alitembelea
makumbusho ya Jeshi la Oman, Chuo cha Ufundi na Teknolojia, chuo kikuu
cha Sultan Qaboos na Baraza la Taifa la Utafiti.
Katika maeneo yote aliyotembelea Mheshimiwa Waziri Shamhuna
alifurahishwa sana na shughuli za taasisi za elimu Oman na kuridhika na
hatua iliyopigwa na Oman katika sekta ya Elimu na mafunzo ya Amali.
Mheshimiwa Waziri Shamhuna pia alitembelea ofisi za Ubalozi wa Tanzania
nchini Oman kujionea shughuli mbalimbali za Ubalozi na pia kuhudhuria
hafla ya chakula cha Usiku kilichoandaliwa kwa heshima yake nyumbani kwa
Mheshimiwa Balozi Ali Ahmed Saleh, Balozi wa Tanzania nchini Oman.
CHANZO: MUHIDIN MICHUZI
No comments:
Post a Comment