Pages

Tuesday, February 18, 2014

KIKONGWE WA MIAKA 90 AJINYONGA KISA KUUGUA KWA MUDA MREFU

RPC Mungi 

Mwandishi Diana Bisangao wa matukiodaima.com
.............................
Watu wawili wafariki dunia katika matukio manne tofauti mkoani Iringa likiwemo la mzee wa miaka 90 kujinyonga kwa kutumia kipande cha kitenge nyumbani kwake.

Akizungumza  ofisini kwake Kaimu Kamanda wa Mkoa wa Iringa Nyigesa Wankyo alithibitisha kutokea kwa tukio hilo lililotokea mnamo tarehe 16 februari majira ya saa 11:04 jioni.

Kaimu kamanda Wankyo alimtaja mzee huyo aliyejulikana kwa jina Dauson Mlonganile mkazi wa kijiji cha Nundwe wilayani Mufindi.
Wankyo alisema chanzo cha tukio hilo ni kuugua kwa muda mrefu kwa mzee huyo.

Katika tukio lingine mtu mmoja mwanaume alikutwa ndani ya shamba la mpunga akiwa amefariki dunia.

Kaimu Wankyo alithibitisha kutokea kwa tukio hilo lililotokea mnamo tarehe 14 februari majira ya saa 2 kamili usiku katika kijiji cha Makifu wilaya ya Iringa vijijini.

Hata hivyo alisema marehemu huyo alikufa kutokana na ugonjwa wa kifafa kumpanda wakati akiendelea na shughuli zake za kilimo zikiwemo za kupanda mpunga, mwili wa marehemu umezikwa na ndugu zake.

Wakati huohuo JESHI la polisi mkoani Iringa linamtafuta mtuhumiwa aliyejulikana kwa jina moja la Cley kwa kosa la kumbaka mwanafunzi jina limehifadhiwa(19) mkazi wa Kihesa na kumsababishia maumivu makali sehemu za siri.

Kaimu Wankyo alisema tukio hilo lilitokea mnamo tarehe 16 februari majira saa 9 kamili mchana na kusema mtuhumiwa huyo alimkaribisha mwanafunzi chumbani kwake na kumvua nguo kisha kumbaka.

Chanzo cha tukio hilo ni tamaa ya mwili na mtuhumiwa bado anatafutwa.

Mbali na matukio hayo matatu, Kaimu Wankyo alisema JESHI la polisi linamshikilia Elisante Benya (27) mkazi wa Frelimo kwa kosa la kukutwa na madawa ya kulevya aina ya bhangi.

Kaimu Wankyo alithibitisha tukio hilo lililotokea tarehe 16 februari majira ya saa 8 kamili mchana maeneo ya kuuzia pombe za kienyeji barabara mbili kata ya makorongoni ambapo mtuhumiwa huyo alikutwa na kete 5 pamoja na msokoto mmoja akiwa ameyahifadhi ndani ya mfuko wa koti alilokuwa amelivaa.


 

No comments:

Post a Comment