Pages

Tuesday, February 18, 2014

Polisi wavamia Waandamanaji Bangkok


Maandamano Bangkok
Habari za hivi punde zinasema kuwa Mamia ya polisi wanakabiliana na waandamanaji ambao wamekita kambi katika afisi za serikali kuanzia mwezi Disemba mwaka jana .
Watu wanasikika wakipiga mayowe huku polisi waliojihami wakifyatua risasi hewani kuwavamia Waandamanaji hao..
Mkuu wa polisi Major-General Adul Dam-rong-sak anasisitiza kuwa ni lazima waandamanaji hao waruhusu uchukuzi na hali ya kawaida kurejea katika jiji hilo Bangkok .
Duru zimeiambia BBC kuwa takriban Waandamanaji 100 wamekamatwa katika operesheni hii ya kwanza tangu mwezi Disemba waandamanaji hao walipovamia afisi za umma mjini Bangkok wakipinga utawala wa Waziri mkuu Yingluck Shinawatra.
Waandamanaji wanadai kuwa Yingluck anatumiwa vibaya na kakake aliyekuwa waziri mkuu wakati mmoja Thaksin Shinawatra ambaye yuko uhamishoni.

Wengi wanaompinga Yingluck wanataka aondoke malakani na badala yake kuchaguliwe baraza la watawala litakaloongoza Thailand hadi uchaguzi ufanyike.
Kiongozi wa upinzani, Suthep Thaugsuban aliwaambia waandamanaji kuwa anapigania utawala na madaraka ya Wathai kurudishia umma .
Uchaguzi uliofanyika mapema mwezi huu ulisusiwa na makundi ya upinzani kwa sababu ilitarajiwa kuwa waziri Yingluck na chama chake wangeibuka washindi.
Yingluck alichaguliwa mnamo mwak wa 2011 kutokana na ufuasi mkubwa kutoka maeneo ya mashambani ya Thailand.chanzo bbc swahili

No comments:

Post a Comment