Mkurugenzi
Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji amewapongeza Wakuu wa Mikoa wa Kanda ya
Ziwa katika juhudi zao za kuhakikisha Kongamano la Uwekezaji Kanda ya
Ziwa linafanyika.
Mikoa
ambayo itashiriki katika Kongamano la Uwekezaji la Kanda ya Ziwa ni
Mwanza, Geita, Mara, Simiyu, Kagera na Shinyanga Kongamano ambalo kwa
pamoja litawakutanisha Wawekezaji pamoja na Serikali katika kujadili
vivutio vya Uwekezaji vinavyopatikana katika mikoa hiyo ya kanda ya
Ziwa.
Kituo
cha Uwekezaji Kimejizatiti kushirikiana na Mikoa katika kuhakikisha kuwa
wawekezaji wanapatiwa huduma zinazohitajika katika Mikoa.
Kituo
cha Uwekezaji na Mikoa wamekubaliana kushirikiana na kuhakikisha
kupatikana kwa Ardhi katika Mikoa ili iweze kuwekwa kwenye Benki ya
Ardhi kwa ajili ya kupatia Wawekezaji na pia kutoa Elimu kwa wananchi
kuhusu sheria na taratibu zinazomtaka muwekezaji kuzifuata kabla ya
kupata ardhi kwa ajili ya uwekezaji.
Kituo
cha Uwekezaji pia kitafanya kazi na Makatibu Tawala wa Mikoa ili kujenga
uwezo ili nao waweze kusimamia utoaji wa huduma vizuri kwa wawekezaji
katika mikoa yao.
Kwa maelezo zaidi kuhusu Kongamano la Uwekezaji Tanga na Vivutio vya Uwekezaji vinavyopatikana Kanda ya Ziwa tembelea tovuti ya www.lakezoneinvestmentforum.go.tz
Pichani ni Mkurugenzi Mtendaji TIC,Bi Juliet R. Kairuki (wa tatu kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na wakuu wa mikoa ya kanda ya ziwa,toka kushoto ni Mhe.
Chief Kishosha Pascal Mabiti (Mkuu wa Mkoa Simiyu); Eng. Evarist
Ndikilo (Mkuu wa Mkoa Mwanza) Mhe. Magalula Said Magalula (Mkuu wa Mkoa,
Geita); Mhe. John Gabriel Tuppa (Mkuu wa Mkoa Mara); Col Phabian
Massawe (Mkuu wa Mkoa Kagera); Mhe. Ali Nassor Rufunga (Mkuu wa Mkoa
Shinyanga)
No comments:
Post a Comment