Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, February 13, 2014

RAIS KIKWETE AFUNGUA KAMPENI MAALUM YA MABANGO YA KUPIGA VITA UUAJI WA TEMBO NA FARU UWANJA WA NDEGE JKN


 Moja ya mabango yaliyozinduliwa na Rais Jakaya Kikwete usiku wa kuamkia leo kwa ajili ya kuhamasisha wananchi kupiga vita mauaji ya Tembo na Faru nchini.


 Rais Jakaya Kikwete (kulia) akibofya kwenye kompyuta kuzindua rasmi  mabango hayo ya kuhamasisha wananchi kupiga vita mauaji ya Tembo na Faru  kwenye  Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam.. Kulia kwake ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Mahamoud  Mgimwa. PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG

 Rais Jakaya Kikwete akizungumza wakati wa uzinduzi wa mabango ya kuhamasisha wananchi kupiga vita mauaji ya Tembo na Far baada ya kuyazindua rasmi kwenye  Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam juzi.

 Moja ya mabango hayo likiwa nje ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam

 Rais Jakaya Kikwete akizungumza wakati wa uzinduzi wa mabango ya kuhamasisha wananchi kupiga vita mauaji ya Tembo na Farubaada ya kuyazindua rasmi kwenye  Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam. Kulia ni OfisaMtendaji Mkuu wa Kampuni ya Jambo Concepts Tanzania Limited, Juma Pinto.Kulia kwake ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Dk. Mahamoud  Mgimwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadick (kushoto kwake).

 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Mahamoud Mgimwa (wa pili kushoto), akiwa na Ofisa Mteendaji Mkuu wa Kampuni ya Jambo Concepts Tanzania Limited (JCTL), Juma Pinto (wa pili kulia) pamoja na Mkurugenzi wa JCTL, Juma Mabakila walipokuwa wakimsubiri Rais Jakaya Kikwete kuzinduz mabango hayo.

 Mfanyakazi wa JCTL Baraka Baraka akiweka sawa mitambo ili matangazo hayo yaonekane vizuri

 Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, alipowasili katika hafla ya uzinduzi wa mabango hayo yatakayosambazwa sehemu mbalimbali nchini.

 Sehemu ya umati ulioshiriki katika hafla hiyo ya uzinduzi wa mabango

 Mmiliki wa Blog ya Wananchi, William Malecela akijadiliana jambo na Juma Pinto


JK akiwa katika hafla hiyo

No comments:

Post a Comment