Watahiniwa wa kike wamefanya vizuri kwa kuchukua nafasi saba
kati ya 10 za juu, huku Shule ya Marian Girls ya Pwani ikiongoza kwa
kuwa na wanafunzi wanne.
Mwanafunzi aliyeongoza ni Robina Nicholaus wa
Shule ya Marian Girls, akifuatiwa na Magrath Kakoko wa St Francis
(Mbeya) wakati wa tatu ni Joyceline Marealle kutoka Shule ya Canossa
(Dar es Salaam).
Wengine ni Safarina Mariki na Abby Sembuche wa
Marian Girls, wakati wavulana pekee kwenye wanafunzi 10 bora ni Sunday
Mrutu kutoka Anne Marie (Dar es Salaam) na Nelson Rugola Anthony na
Emmanuel Mihuba Gregory wa Kaizirege (Kagera).
Wanaofuata ni Janeth Urassa kutoka Marian Girls (Pwani) na Angle Ngulumbi wa St Francis (Mbeya).
Wasichana 10 bora
Wasichana waliofanya vizur kwenye mtihani huo
wameongozwa na Robina Nicholaus (Marian Girls), Magrath Kakoko (St
Francis), Joyceline Leonard Marealle (Canossa), Safarina W Mariki, Abby T
Sembuche na Janeth Urassa (Marian Girls).
Wengine ni Angle Ngulumbi (St Francis), Getrude
James Mande wa Precious Blood (Arusha), Violet Mwasenga wa St Francis na
Catherine Swai kutoka Marian Girls.
Wavulana 10 Bora
Wavulana waliofanya Vizuri ni Sunday Mrutu wa Anne
Marie, Nelson Rugola Anthony na Emanuel Mihuba Gregory wote kutoka
Kaizirege, Razack Hassan wa St Matthew’s (Pwani) na Hamis Msangi kutoka
Eangles (Pwani).
Wengine ni Joshua Zumba wa Uwata (Mbeya), Brian
Laurent na Mohamed Ally wa Marian Boys (Pwani), Shahzill Msuya wa St
Amedeus (Kilimanjaro) na Shabani Hamisi Maatu wa Mivumon Islamic
Seminary (Dar es Salaam).
Shule za serikali hoi
Matokeo yanaonyesha kuwa shule kumi za kwanza ni za binafsi tu na shule za Serikali zimeanguka vibaya.
Shule bora ni St. Francis Girls ya Mbeya, Marian
Boys ya Pwani, Feza Girls ya Dar es Salaam, Precious Blood ya Arusha,
Canossa ya Dar es Salaam, Marian Girls ya Pwani, Anwarite Girls ya
Kilimanjaro, Abbey ya Mtwara, Rosmin ya Tanga na Don Bosco Seminary ya
Iringa.
Katika shule zenye watahiniwa chini ya 40 shule
iliyoongoza ni Kaizirege ya Kagera, Alliance Girls ya Mwanza, Thomas
More Machrina ya Dar es Salaam, Mwanza Alliance ya Mwanza na Queen of
Apostles Ushirombo Seminary ya Geita.
Nyingine ni St Joseph Kilocha Seminary ya Njombe, Bethelsabs Girls ya Iringa, St Mary Junior Seminary ya Pwani, Maua Seminary ya Kilimanjaro na Hellen’s ya Dar es Salaam.
Nyingine ni St Joseph Kilocha Seminary ya Njombe, Bethelsabs Girls ya Iringa, St Mary Junior Seminary ya Pwani, Maua Seminary ya Kilimanjaro na Hellen’s ya Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment