Afisa
mmoja wa serikali ya Libya na watu wengine kumi wameuawa kufuatia
kuanguka ndege moja ya kijeshi karibu na Tunis mji mkuu wa Tunisia.
Ndege hiyo ilikuwa imebeba wagonjwa.
Sheikh
Meftah Daouadi, Naibu Katibu Mkuu katika Wizara ya Mashahidi ya Libya
na abiria kumi pamoja na mhudumu mmoja wa ndege wamefariki dunia baada
ya ndege hiyo aina ya Antonov kupata ajali wakati ikijaribu kutua.
Shirika
la habari la Tunisia limeripoti kuwa ndege hiyo ya Libya ilianguka
baada ya rubani kujaribu kutua katika shamba karibu na mji wa Grombalia
lililoko umbali wa karibu kilomita 40 kusini mwa Tunis mji mkuu wa
Tunisia.
Tawfik
Rahmouni msemaji wa masuala ya ulinzi wa Tunisia amesema kuwa mhudumu
wa ndege hiyo ya kijeshi ya Libya aliwasiliana na uwanja wa ndege wa
Carthage wa Tunisia kabla ya ajali hiyo akisema kuwa injini za ndege
zimeshika moto.
No comments:
Post a Comment