Pages

Friday, February 28, 2014

MKOSAJI MKUU WA HAKI ZA BINADAMU NI SERIKALI - JAJI MSTAAFU MIHAYO


DSC_0259
Mjumbe wa Bodi ya Mtandao wa watetezi wa Haki za Binadamu nchini (Tanzania Human Rights Defenders Coalition) Dkt. Hellen Kijo Bisimba akitoa neno la ufunguzi wakati wa warsha ya siku moja iliyowakutanisha watetezi wa Haki za Binadamu nchini na Jeshi la Polisi jijini Dar leo.
.Asema dunia nzima inajua mvunjifu wa kwanza wa haki za binadamu ni dola
.Polisi pia ni binadamu wanahitaji kutetewa na mitandao ya haki za binadamu nchini

Na Damas Makangale, MOblog Tanzania
MKOSAJI na mvunjifu mkubwa wa haki za binadamu ni serikali kutokana na mazingira halisi ya utendaji na mfumo mzima wa utawala katika serikali nyingi duniani. Imeelezwa.

Akizungumza kwenye warsha ya siku moja iliyoandaliwa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu nchini, Tanzania Human Rights Defenders Coalition (THRDC) kwa wakuu na makamanda wa Jeshi la Polisi nchini, Jaji Mstaafu, Thomas Mihayo amesema kwa mfumo wa utawala katika nchi nyingi duniani mkosaji mkuu wa haki za binadamu ni serikali.

“dunia nzima inajua kwamba serikali ndio mkosaji mkuu wa haki za binadamu na maana halisi ya serikali ni dola na mahakama tu kwisha,” amesema Jaji Mihayo
Jaji Mihayo amesema kuwa kwa hali ya kawaida dola ikimkamata mtu au mhalifu lazima mpeleke katika mahakama ili sheria ichukue mkondo wake wa kawaida.
DSC_0316
Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Abdurahman Kaniki, akitoa hotuba yake ya ufunguzi kwa niaba ya IGP Ernest Mangu, kwenye warsha ya siku moja iliyowakutanisha viongozi waandamizi wa Jeshi hilo na watetezi wa Haki za Binadamu nchini.

Kwa upande wake, Mjumbe wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu, Dkt Helen Kijo Bisimba akitoa neno la ufunguzi amesema warsha hiyo inatoa fursa nzuri kwa watetezi wa haki za binadamu na Jeshi la Polisi kuboresha kazi zao za utetezi wa haki za binadamu nchini. Amesema kwa ujumla haki za binadamu hazipewi bali ni haki ya msingi ambayo mtu anazaliwa nayo ili zinaminywa aidha kupitia mtu kwa mtu au taasisi au mfumo wa utawala.

“Kazi za watetezi wa haki za binadamu na Jeshi la Polisi zinaendama na msingi ni utetezi wa haki za binadamu pamoja na mali zao,” alisisitiza
Naye, Mratibu wa kitaifa wa Mtandao huo, Onesmo Olengurumwa akiwasilisha mada yake ya (The Concept of Protection and Security Management for Human Rights Defenders and Social Organization) amesema kuwa taaluma inaweza kutumika kutetea haki za binadamu katika maeneo mengi hapa duniani.
DSC_0334 DSC_0379
Jaji Mstaafu Thomas Mihayo akizungumza na Makamanda wa Jeshi la Polisi nchini, umuhimu wa kushirikiana kati ya Jeshi hilo na Asasi za kutetea Haki za Binadamu ili kuleta tija katika nyanja za kiuchumi, kijamii na kisiasa.
Amesema pia kupitia mada hiyo kwamba jamii inadhani kwamba anayepaswa kutetewa ni mwananchi tu lakini pia hata polisi naye ni binadamu anapaswa kuwa na mtetezi pale ambapo haki yake ya msingi inapovunjwa.

“Mpaka sasa Tanzania haina sheria yeyote inayomlinda mtetezi wa haki za binadamu lakini tunaendelea na mchakato na ni matumaini yetu serikali itaridhia kuwa na sheria hiyo hapa nyumbani,” alilisitiza
Naibu Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi nchini, Abdurahman Kaniki amesema kuwa jeshi la polisi nchini litaendelea kuimarisha mahusiano kati ya jeshi hilo na watetezi wa haki za binadamu nia ni kudumisha amani na utulivu nchini.
DSC_0325
Sehemu ya makamishina na makamanda wa mikoa na maafisa waandamizi wa Jeshi la Polisi nchini wakifuatilia mada mbalimbali kwenye warsha hiyo ya siku moja jijini Dar es Salaam.

“majukumu ya jeshi la polisi na watetezi wa haki za binadamu nchini yanafanana kwa kila hali ni kulinda na kutetea haki za wananchi na mali zao,” amesema Naibu IGP Kaniki,Kamishina Kaniki alilisitiza kwamba ni muhimu wadau wote kuzingatia sheria za nchi, taratibu na kanuni katika kutafuta haki mbalimbali ili kudumisha amani na utulivu nchini.

“nachukua nafasi kuwakaribisha wadau wote wa haki za binadamu na makundi mengine kushirikiana na jeshi la polisi katika kulinda na kutetea haki za binadamu nchini,” alisisitiza.Kamanda wa Polisi Arusha, RPC Liberatus Sabas amesema kwa muda mrefu watu wa utetezi wa haki za binadamu na makundi mengine huwa wanasahau kwamba polisi pia ni binadamu nao wanahitaji utetezi kutoka kwa watetezi hao wa haki za binadamu.
DSC_0375 DSC_0417
Naibu Inspekta General wa Jeshi la Polisi nchini, Abdurahman Kaniki (kushoto), Mratibu wa THRDC Taifa, Onesmo Olengurumwa (katikati) pamoja na Mkurugenzi wa Mafunzo na Oparesheni, Kamishina Paul Chagonja wakifuatilia mbalimbali ilizokuwa ikitolewa na washiriki wa warsha hiyo.

DSC_0291
Mratibu wa THRDC Taifa, Onesmo Olengurumwa akiwasilisha mada yake juu ya Ulinzi na utawala wa haki za binadamu kwa mashirika ya watetezi wa Haki za Binadamu pamoja na Polisi.
DSC_0355
Pichani juu ni Meza kuu na chini ni Baadhi ya Wakuu na Makamishina wa Jeshi la Polisi nchini wakifurahia jambo wakati wa uwasilishwaji wa mada mbalimbali kwenye warsha ya siku moja iliyowakutanisha viongozi waandamizi wa Jeshi hilo na watetezi wa Haki za Binadamu nchini.
DSC_0362 DSC_0413
Kamishina wa kanda maalum ya Dar es Salaam, RPC, Sulemain Kova akichangia mada katika warsha ya siku moja kuhusu Haki za Binadamu na ushirikiano kati ya Jeshi la Polisi na watetezi wa Haki za Binadamu nchini.
DSC_0397
Kamanda wa Polisi, Arusha Liberatus Sabas akizungumza umuhimu wa kujali pia askari polisi kwa sababu na wao pia ni Binadamu wanahitaji utetezi kutoka kwa mashirika yasiyo ya kiserikali yanayotetea Haki za Binadamu nchini.
DSC_0390
Kamanda wa Polisi, Lindi, RPC Zeloithe Stephen akitoa nasaha kuhusu miiko na kanuni za Jeshi la Polisi jinsi zinavyotetea na kulinda Haki za Binadamu (Police General Order).
DSC_0438
Picha ya pamoja kati ya viongozi waandamizi wa Jeshi la Polisi nchini na mgeni rasmi Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi nchini.
DSC_0441
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Bi. Usu Malya (kulia) akiteta jambo na Kamishina wa kanda maalum ya Dar es Salaam, RPC, Sulemain Kova baada ya kupiga picha ya pamoja


 

No comments:

Post a Comment