JAMHURI
YA MUUNGANO TANZANIA
WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII
|
TANGAZO
Katibu Mkuu, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii anapenda kuwatangazia Wauuguzi wa ngazi ya Astashahada na ngazi ya Stashahada
waliohitimu mafunzo mwaka 2013 wawasilishe
maombi ya kupangiwa vituo vya kazi. Waombaji wanatakiwa kupendekeza maeneo
matatu wanayotaka wapangiwe kazi.
Maeneo yenye nafasi za kazi
yameainishwa kwenye tangazo la kazi kwenye tovuti ya Wizara ya Afya na Ustawi
wa Jamii (www.moh.go.tz).
Maombi wayawasilishwe kwa Katibu
Mkuu, Wizara ya Afya na Ustawi wa
Jamii kwa anuani ya hapa chini kabla
ya tarehe 14 Machi, 2014.
Katibu Mkuu,
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,
S.L.P. 9083,
DAR ES SALAAM.
No comments:
Post a Comment