Wagombea wakiwa katika mapozi kabla ya kuanza kwa zoezi la kupiga kura halijaanz |
Baadhi ya wajumbe wa mkutano huo wakipiga makofi wakati wakisubiri zoezi la upigaji kura lianze |
wageni rasmi |
Msanii wa CCM Ally Bin Ahamed maarufu kwa jina la mpemba asilia akitoa mashairi ya kuipongeza CCM |
wajumbe wengine |
Wagombea nao wakijifariji kwa makofi ya wajumbe
KAIMU
Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa, Hassan Mtenga
amewasihi wajumbe wa mkutano huo kumchangua mgombea anayoonekana
kukubalika kwa asilimia 60 kwa wapiga kura.
"Falsafa
ya chama kwanza, mtu baadaye lazima tuipime vizuri, tunahitaji ushindi
na ili tupate ushindi lazima tuangalie wananchi wanataka nini," alisema.
Akifungua mkutano huo, Mtenga aliwataka wagombea ndani ya chama hicho wawe na utamaduni wa kukubali matokeo kwa afya ya chama.
Alisema
wagombea wote tisa waliojitokeza katika kura hizo za maoni wana sifa za
kuwa wabunge na akawataka wajumbe kutumia busara zaidi wakati wakifanya
uamuzi.
Alisema mchakato wa kura za maoni ndani ya chama hicho umecchukua siku mbili hali itakayosaidia kukinusuru chama na mipasuko.
“Tulikuwa
na kawaida ya kufanya kura za maoni kwa zaidi ya mwezi mmoja; hali hiyo
ilikuwa ikiwaacha wagombea katika majeraha makubwa ya matumizi ya
fedha,” alisema.
Alisema
majeraha hayo yamekuwa yakichangia hasira kwa wagombea walioshindwa
ambao badala ya kukisaidia chama kipate ushindi, hufurahia kinapopoteza
nafasi.
Alisema
kwa mtaji walionao, CCM wana hakika na ushindi wa kishindo katika jimbo
hilo lililoachwa wazi na aliyekuwa Waziri wa Fedha, Dk William Mgimwa.
Waliojitokeza kupitia katika chama hicho ni pamoja na Jackson Kiswaga, Hafsa Mtasiwa, Godfrey Mgimwa.
Wengine ni Gabriel Kalinga, Peter Mtisi, Edward Mtakimo, Bryson Kisaba, Msafiri Pagamila na Thomas Mwakoka.
|
No comments:
Post a Comment