Pages

Thursday, February 13, 2014

MTOTO MMOJA AMEFARIKI DUNIA BAADA YA KUANGUKIWA NA UKUTA WA NYUMBA KATIKA ENEO LA MAJENGO MANISPAA YA DODOMA.


Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoani Dodoma David Misime amesema chanzo cha kifo cha Mtoto huyo mwenye umri wa miaka miwili ni ubovu wa nyumba na ukuta uliokuwa umeloana kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha  jambo lililopelekea kuanguka na kusababisha kifo hicho.

Aidha Kamanda Misime amesema ukuta huo uliwaangukia Bi Hadija Mtoro  mwenye umri wa miaka 80 na Marehemu wakiwa wanapika chakula cha jioni  majira ya saa moja na dk 50 ambapo baada ya kuangukiwa mama huyo alipiga kelele kuomba msaada ndipo majirani wakafika eneo La tukio na kutoa msaada huo.

Baada ya majirani kuondoa matofali yaliyokuwa juu yao waliwabeba majeruhi na kuwapeleka katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma ndipo ikabainika kuwa mtoto huyo amefariki dunia kwa uchunguzi wa daktari.Na Dodoma Fm

No comments:

Post a Comment