Mtoto Anastazia Jumanne akiwa amefungwa mikono yake kwenye pikipiki kwa mpira.
Mtoto Anastazia Jumanne (12) ambaye ni mwanafunzi wa shule ya msingi katika wilaya na mkoa wa Geita amefanyiwa ukatili wa kutisha baada kufungwa mpira kwenye pikipiki na baba yake mzazi na kisha kuanza kumburuza mtaani.
Tukio
hilo la kusikitisha limetokea jana majira ya sa tatu asubuhi katika moja
ya mitaa ya mjini humo ambapo inadaiwa kuwa binti huyo anayesoma darasa
la nne katika shule hiyo alikataa kwenda shule kitendo ambacho
kilimkasirisha baba yake aitwaye Jumanne Nkoyogi ambaye pia ni
mfanyabiashara wa samaki mjini Geita.
Mashuhuda
wa tukio hilo baada ya kuona asubuhi hiyo mtoto huyo akiburuzwa huku
amefungwa kwenye pikipiki walianza kupiga makelele na kukusanyana kwa
lengo la kumkamata baba huyo aliyekuwa anafanya unyama huo.
Baada ya
kumkamata na kumtia kumtia mikononi mwao walimpeleka kwenye ofisi ya
sungusungu iliyopo Ihayabuyaga kata ya Kalangalala na kufungiwa humo kwa
usalama wake.
Akizungumzia
tukio hilo katibu wa sungusungu kata ya Kalangalala aliyempokea
mtuhumiwa huyo Abel Richard alisema tukio hilo liliwafanya wananchi
kujaa jazba dhidi ya mzazi huyo na kutaka kumpiga.
Alisema
mzazi huyo kwa sasa anashikiliwa na jeshi la polisi wilayani Geita baada
ya katibu huyo kuwasiliana na uongozi wa jeshi hilo na kuwatuma askari
kwake kumchukua haraka kwa usalama wake.
Afisa
upelelezi wa mkoa wa Geita Simon Pasua amekiri kuwepo kwa tukio hilo na
kusema kuwa mtuhumiwa anashikiliwa na jeshi la polisi hadi sasa kwa
upelelezi zaidi.
Na Valence Robert-Geita
No comments:
Post a Comment