Maskofu
wakuu katika kanisa moja nchini Uingereza wamewaambia viongozi wa dini
kwamba hawataruhusiwa kuingia katika ndoa za jinsia moja,na kusema kuwa
hawatakubali viongozi wa dini masenge kwenda kinyume na maagizo hayo. Viongozi
wa dini wa kanisa la Ki-Anglikana wanakubaliwa na kanisa hilo kuingia
katika uhusiano wa kimapenzi lakini kwa maelewano kwamba hawatashiriki
ngono.
Katika mwelekeo wao, maaskofu hao pia wamepiga marufuku maombi yoyote maalum kwa wanadoa wa jinsia moja licha ya ripoti rasmi ya kanisa hilo kupendekeza kwamba viongozi wa dini wanaweza kufanya hivyo iwapo wanajihisi. Hatahivyo amesema kuwa viongozi wa dini wanapaswa kutoa maombi yasio rasmi kwa wanandoa walio katika uhusiano wa jinsia moja.
Chanzo - BBC Swahili
No comments:
Post a Comment