Pages

Wednesday, February 19, 2014

PROFESA ELISANTE: MILANGO IKO WAZI KWA VIONGOZI WA VYAMA

PIX1Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mchezo wa Tennis Tanzania(TTA) Bw. William Kallaghe(kushoto) alipokutana naye ofisini kwake jana jijini Dar es Salaam.PIX2Katibu Mkuu wa Chama cha Mchezo wa Tennis Tanzania(TTA) Bw. William Kallaghe(kushoto) aakimwelezea jambo Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel alipomtembelea ofisini kwake jana jijini Dar es Salaam.PIX3Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo wa Wizara ya Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Leonard Thadeo(kulia) akifafanua jambo wakati wa kikao cha pamoja baina ya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel(katikati) na Katibu Mkuu wa Chama cha Mchezo wa Tennis Tanzania(TTA) Bw. William Kallaghe(kushoto) jana jijini Dar es Salaam.
PIX4Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Michezo wa Wizara ya Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Juliana Yassoda (kushoto) akifafanua jambo wakati wa kikao cha pamoja baina ya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel(kulia) na Katibu Mkuu wa Chama cha Mchezo wa Tennis Tanzania(TTA) Bw. William Kallaghe(katikati) jana jijini Dar es Salaam.PIX5Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (kulia) akiagana na Katibu Mkuu wa Chama cha Mchezo wa Tennis Tanzania(TTA) Bw. William Kallaghe(kushoto) mara baada ya kumaliza mazungumza yao jana jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Michezo wa Wizara ya Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Juliana Yassoda (katikati) akiteta jambo mara baada ya kikao chao kumalizika, kulia Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo nchini Bw. Leonard Thadeo na kushoto ni Katibu Mkuu wa Chama cha Mchezo wa Tennis Tanzania(TTA) Bw. William Kallaghe jana jijini Dar es Salaam.
PIX7
Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Leonard Thadeo, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijina, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel, Katbu Mkuu wa Chama cha Mchezo Tennis Tanzania (TTA) Bw. William Kallaghe na Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Michezo Bi. Juliana Yassoda wakiwa katika p[icha ya pamoja mara baada ya kumaliza kikao chao jana jijini Dar es Salaam.
Picha zote na Frank Shija – Wizara ya Habari.
……………………………………………………………………………………………
Na  Frank Shija – WHVUM
Viongozi wa vyama vya michezo nchini wametakiwa kutmia fursa zilizopo kukutana na  viongozi wa Serikali ili kujadili kwa pamoja namna ya kuendeleza sekta ya michezo hapa nchini.
Rai hiyo imetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel alipokutana Katibu Mkuu wa Chama cha Mchezo wa Tennis Tanzania (TTA) Bw. William Kallaghe alipomtembele ofisini kwake jana jijini Dar es Salaam.
Profesa Elisante alisema kuwa ni vyema viongozi wa vyama vya michezo kushirikiana na Serikali katika kutafuta namna ya kuendeleza michezo nchini badala ya kukaa na kulalamikia pembeni.
Aidha amesema kuwa milango iko wazi kwa viongozi wa vyama vuya michezo kufika katika ofisi za Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo na kuongeza kuwa atafarijika sana akiona kasi ya viongozi hao kutembelea Wizarani hapo ikiongezeka.
“Natao wito kwa viongozi wa vyama vya michezo nchini wajenge utamaduni wa kushirikiana na Serikali kupitia Wizara hii ili kutafuta namna na njia bora ya kuendeleza sekta ya michezo hapa nchini badala ya kukaa pembeni na kuiilaumu Serikali, kwakweli hii si sawasawa” Alisema Profesa Elisante.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Chama cha Mchezo wa Tennis Tanzania (TTA) Bw. William Kallaghe ameipongeza Serikali kupitia Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kwa ushirikiano ambao wamekuwa wanautoa kwa vyama vya michezo hapa nchini na kusema kuwa hii inaleta faraja kuwafanya kutokuwa wapweke.
Kallaghe aliongeza kuwa ni vyema sasa viongozi wa vyama vya michezo wakatambua umuhimu wa kufanya kazi kwa karibu na Serikali ili kuleta ufanisi katika kutekeleza majukumu yao mbalimbali.
 
Aliongeza kuwa atahakikisha anahamasisha viongozi wenzake kutumia fursa za kukutana na viongozi wa Serikali ili kukaa meza moja na kujadiliana namna ya kuboresha sekta ya michezo hapa nchini.

No comments:

Post a Comment