Pages

Wednesday, February 19, 2014

3 wauawa katika mashambulizi Beirut

Majeruhi wa mashambulizi mjini Beirut
Kumetokea mashambulio mengine ya mabomu Kusini mwa mji mkuu wa Lebanon, Beirut.
Maafisa wa usalama wanasema washambulizi wawili wa kujitoa muhanga walijilipua karibu na kituo cha kitamaduni cha Iran na kuwauwa watu 3 huku wakiwajeruhi wengi.
Kituo cha televisheni cha Hezbollah al-Manar pamoja na duru za kiusalama , zimesema kuwa kilichotokea ni mashambulizi mawili ya kigaidi huku mshambuliaji wa kwanza akilipua mabomu aliyokuwa ametega ndani ya gari. Punde baada ya shambulizi hilo, lengine la pili likatokea.Ni shambulizi la hivi karibuni katika msururu wa mashambulizi katika eneo ambalo ni ngome ya kundi la dhehebu la kishia la Hezbollah.
Bomu la pili lilikuwa limetegwa juu ya pikipiki.
Milipuko hiyo imesababisha uharibifu mkubwa wa maduka na majengo katika eneo hilo.
Ubalozi wa Iran, ulisema kuwa hapakuwa na majeraha makubwa kwa wafanyakazi wake wa kituo chake cha kitamaduni ambacho huenda kililengwa kwa mashambulizi.

Mabomu hayo pia yalililipukia karibu na ofisi za ubalozi wa Kuwait, lakini umesema kuwa wafanyakazi wake hawakujeruhiwa.
Mnamo mwezi Novemba, zaidi ya watu 20 waliuawa katika mashambulizi kama haya ya kujitoa mhanga dhidi ya ubalozi wa Iran.
Tangu hapo kumeshuhudiwa mashambulizi ya mara kwa mara licha ya usalama kudhibitiwa vikali
CHANZO BBCSWAHILI

No comments:

Post a Comment