Mshehereshaji Meneja wa Maadili wa Baraza la Habari Tanzania(
MCT), Bw. Allan Lawa, akiwakaribisha wageni waalikwa kwenye maadhimisho
ya siku ya Redio Duniani yaliyofanyika Kitaifa mkoani Dodoma.
Maadhimisho hayo yameandaliwa na Baraza la Habari Tanzania (MCT) na
kufadhiliwa na UNESCO.
Na Mwandishi Wetu, Moblog Tanzania, Dodoma
UMOJA
wa Mataifa umesema kwamba bado redio nyingi duniani ziko nyuma katika
kuhabarisha habari za usawa wa jinsia na sauti za wanawake na wasichana
hazipati nafasi ya kutosha katika matangazo ya kila siku katika vyombo vingi vya habari.
Akisoma ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bw, Ban Ki-Moon na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bi Irina Bokova, katika maadhimisho ya siku ya Radio
Duniani jijini Dodoma, Afisa Habari wa umoja wa Mataifa, Bi Usia Nkhoma
Ledama amesema mbaya zaidi katika bodi za mashirika ya vyombo vya
habari wanawake ni robo tu ya wanabodi.
“Ninavihimiza vituo vya redio kuwatambua kwa usawa wanawake kama wafanyakazi na kama wasikilizaji wake,”“Maadhimisho
ya mwaka huu yanatukumbusha wajibu wa watangazaji wa redio duniani kote
kuipaza sauti ya wanawake na kuthamini nafasi ya wanawake katika
mashirika ya utangazaji,” akisoma taarifa hiyo
Bi
Usia akisoma taarifa hiyo amesema Radio pia inaweza kusaidia sana
kumaliza unyanyapaa dhidi ya wanawake na programu zisizozingatia usawa
wa kijinsia kwa wote.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Rehema Nchimbi akisalimiana na Mkufunzi wa Redio za Jamii kutoka Unesco, Mama
Rose Haji Mwalimu meza kuu wakati wa maadhimisho ya siku ya Redio
Duniani yaliyofanyika Kitaifa mkoani Dodoma. Katikati ni Katibu Mtendaji
wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Bw. Kajubi Mukajanga.
Amesema
kwenye hotuba hiyo ya wakuu wa Umoja wa Mataifa kwamba hii ni fursa
kwao wote, kusherehekea Siku Ya Radio Duniani kwa kuwatambua wanawake na
kufanya yale yaliyo ndani ya uwezo wao kuzilea sauti mpya za kesho.
Kwa
upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO Bi Irina Bokova amesema na
ninanukuu; Katika Siku ya Redio Duniani, tunaadhimisha chombo ambacho
kinategemewa zaidi na watu wengi, wanaume kwa wanawake, duniani kote.
Redio huwapa sauti wale wasio na sauti, husaidia kuelimisha watu wasio
na elimu, na inaokoa maisha wakati wa majanga.
Akisoma
taarifa hiyo amesema ikiwa ni chachu ya uhuru wa kujieleza na
ushirikishwaji wa wengi, redio ni muhimu katika kujenga jamii yenye
uelewa na kukuza heshima na uelewano baina ya watu.
Katibu
Mtendaji wa Baraza la Habari (MCT), Bw.Kajubi Mukajanga akizungumza
machache kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt.
Rehema Nchimbi.Ujumbe
huo wa Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO ulisisitiza kwamba Radio ni muhimu
zaidi katika kukuza usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake.
“Tangu
wakati wa watendaji waanzilishi mwanzoni mwa karne ya 20 hadi hawa wa
sasa wanaoripoti kutoka kwenye maeneo yenye vita, wanawake wamefanya
kazi kubwa katika ukuaji wa redio,Kama waandishi wa habari wa kiraia,
maripota, watengenezaji vipindi, mafundi, na watu muhimu wanaofanya
maamuzi, wanawake wanafanya kazi katika kila ngazi ya sekta ya
utangazaji kuhakikisha ubadilishanaji huru wa maoni, habari na mawazo
kupitia masafa,” ilisema taarifa hiyo.
Bi
Usia amesema kupitia ujumbe huo kwamba ni kwa sababu hiyo UNESCO
inafanya kazi duniani kote kuendeleza radio kama chombo huru na
kinachoshirikisha watu wengi kwa ajili ya wanaume na wanawake, na
kutengeneza mazingira salama zaidi kwa waandishi wa habari wote, kwa
kutambua kwa namna ya pekee vitisho kwa waandishi wa habari wanawake.
Pichani
juu na chini ni Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Rehema Nchimbi
akizungumza na wadau wa sekta ya Habari nchini kwenye maadhimisho ya
siku ya Redio Duniani yaliyofanyika Kitaifa mkoani Dodoma.
Mgeni
rasmi katika maadhimisho hayo alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dr.Rehema
Nchimbi ambaye aliwaasa waandishi kutangaza vipindi vyenye manufaa kwa
jamii ili kusaidia kusukuma maendeleo.
“Tungependa kusikia vipindi vya maendeleo zaidi katika redio kuliko vipindi vya muziki,”alisema.Naye
Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari (MCT)Kajubi Mukajanga alisema
maadhimisho hayo yamewashirikisha washiriki kutoka nchi nzima na
yanalenga kuwakumbusha wajibu watangazaji wa redio juu ya nafasi ya
radio katika kuelimisha jamii.
Afisa
Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa(UNIC), Bi. Usia
Nkhoma Ledama, akisoma Ujumbe kutoka kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa
Bw. Ban Ki-moon na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la
Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Bi Irina Bokova katika Maadhimisho
ya Siku ya Redio Duniani.
Mchokonozi wa Mada na Mkufunzi wa Redio za Jamii kutoka Unesco Mama Rose
Haji Mwalimu akiwasilisha mada inayosema kutumia fursa ya Redio kukuza
usawa wa Kijinsia na kuwawezesha Wanawake katika Uongozi.
Meneja
Machapisho, Utafiti na Uhifadhi Hati wa Baraza la Habari Tanzania
(MCT), Bw. John Mireny, akitoa maelezo mafupi kuhusu machapisho
mbalimbali ya baraza hilo yanayotoa mafunzo mbalimbali ya tasnia ya
habari.
Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Rehema Nchimbi akizindua machapisho ya Baraza la Habari Tanzania (MCT) kwenye maadhimisho ya siku ya Redio Duniani. Kushoto ni Mkufunzi wa Redio za Jamii kutoka Unesco Mama Rose Haji Mwalimu na Kulia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari (MCT), Bw.Kajubi Mukajanga.
Baadhi
ya Wadau wa Sekta ya Habari, Watangazaji na waandishi wa Redio za Jamii
nchini wakiwa kwenye maadhimisho ya siku ya Redio Duniani yaliyofanyika
Kitaifa mkoani Dodoma.
Afisa
Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi. Usia
Nkhoma Ledama akifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye maadhimisho ya Siku
ya Redio Duniani.
Wadau wa UNESCO na MCT.
Baadhi
ya waandishi wa habari wa Redio za jamii nchini na wadau wa sekta ya
habari wakichangia maoni wakati wa majadiliano ya kuzungumzia changamoto
zinazozikabili redio za jamii nchini.
Mgeni
rasmi Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Rehema Nchimbi akiwa kwenye picha ya
pamoja na wadau wa Sekta ya habari walihudhuria maadhimisho ya siku ya
Redio duniani yaliyofanyika Kitaifa mkoani Dodoma kwa mara ya kwanza.
No comments:
Post a Comment