Pages

Friday, February 14, 2014

Yanga SC yakubali kuweka kambi Chamazi

Na Khadija Mngwai
UONGOZI wa Klabu ya Yanga umefunguka kuwa upo tayari kuweka kambi Chamazi kufuatia ofa waliyoitoa Azam ya kuwataka wakaweke kambi huko kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa raundi ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly ya Misri.

Inaelezwa kuwa wiki iliyopita uongozi wa Azam FC ulikataa ombi la Al Ahly kuweka kambi kwenye eneo lao hilo pindi watakapokuja nchini kucheza dhidi ya Yanga katika hatua hiyo baada ya kufanikiwa kuitoa Komorozine.
TUNAOMBA BOFYA HAPA NA ULIKE PAGE YETU KWA HABARI NYINGI MOTOMOTO(USIPITWEEEE)
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Abdallah Bin Kleb ameliambia gazeti hili kuwa hawawezi kuiachia ofa kama hiyo kwa kuwa mtazamo wao ni kuona wanafanikiwa kufanya vizuri katika mechi hiyo.
“Mtu yeyote hawezi kukataa ofa kama hiyo, iwapo Azam wameamua kutusaidia sisi tupo tayari ila tunamsikiliza mwalimu Hans Van Pluijm anahitaji kambi ya aina gani ili kuweza kujiandaa.
“Mwalimu ndiye anayejua aina ya timu anayotarajia kukutana nayo, hivyo uongozi unamwachia kila kitu na yeye ndiye atakayetoa maamuzi,” alisema Bin Kleb.

No comments:

Post a Comment