Inawezekana wakati unatembea njiani ukaona wanaume
au watoto wadogo wa kiume wakiwa na matiti tena makubwa ambapo watu
wengi huchukulia kama ni kawaida. Kitaalamu, tatizo hilo hujulikana
kama, gynecomastia nalo ni kukua kuliko kawaida kwa tishu ya kwenye titi
inayojulikana kama glandular tissue.
Tatizo hili huonekana zaidi kwa watoto wachanga
na wanaume walio katika umri wa kubalehe, lakini pia huonekana kwa watu
wazima na wazee.
Ukubwa wa tatizo
Asilimia 60-90 ya watoto wachanga wanapata tatizo
hili la kukua kwa matiti kwa mpito linalojulikana kitaalamu kama,
transient gynecomastia kutokana na kuwepo kwa kichocheo cha aina ya
estrogen kwa wingi wakati wa ujauzito wa mama.
Kati ya asilimia 4-69 ya vijana walio katika umri
wa kubalehe imeonekana wanapata tatizo hili kutokana na kuwepo kwa
wingi kwa kimeng’enyo aina ya estradiol. Mara nyingi huonekana katika
umri kati ya miaka 10-12 na hupotea taratibu ndani ya miezi 18, si
kawaida yake kuonekana kwa vijana walio na umri wa zaidi ya miaka 17.
Asilimia 24-65 ya watu wazima hupatwa na tatizo
hili, hii hutokana na kubadilishwa kwa wingi kwa kichocheo aina ya
testosterone kuwa estradiol na kutolewa kwa uchache kwa kichocheo hiki
cha testosteron kutoka kwenye korodani ziazoanza kuzeeka..Ikumbukwe ya
kwamba kichocheo hiki testosteron hutengenezwa katika korodani.
Kichochezi cha testosteron ndicho kichochezi kikuu cha kiume
kinachowezesha tabia za kimwili za kiume.
Nini hutokea?
Kuongezeka ukubwa wa matiti kwa wanaume hutokana
na kuharibika kwa mfumo wa vichocheo unaojulikana kitaalamu kama,
estrogen-androgen balance na hivyo kusababisha estrogen kutolewa kwa
wingi ama kuongezeka kwa msisimko wa matiti kwa kiwango cha zaidi ya
kawaida kwa kichocheo aina ya estrogen kilicho kwenye mzunguko wa damu.
Kichocheo hiki husababisha chembechembe
zinazojulikana kama ductal epithelia kuongezeka kwa wingi, kurefuka na
kugawanyika, kuongezeka kwa chembechembe za mafuta na kuongezeka kwa
mfumo wa damu kwenye matiti hutengenezwa kutoka kwenye vichocheo vya
testosteron na androgen kwa kutumia kimeng’enyo kinachojulikana kama
aromatase.
Aina za tatizo hili
-Puffy nipples –Kuongezeka ukubwa wa chuchu za matiti kutokana na kuongezeka kwa tishu aina ya glandular.
No comments:
Post a Comment