WANAWAKE WAWILI WAUAWA NA WAUME ZAO KUTOKANA NA WIVU WA KIMAPENZI.
WANAWAKE
WAWILI WALIUAWA NA WAUME ZAO KATIKA MATUKIO MAWILI WILAYANI CHUNYA.
KATIKA TUKIO LA KWANZA LILILOTOKEA MNAMO TAREHE 06.02.2014 MAJIRA YA SAA
07:00HRS ASUBUHI HUKO KATIKA KIJIJI CHA SHOGA WILAYA YA CHUNYA MKOA WA
MBEYA MWANAMKE ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA AGNES DAUD (32) MKAZI WA KIJIJI
CHA SHOGA ALIKUTWA AMEUAWA NA MUME WAKE ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA
THOMAS @MSUKUMA KWA KUMKATA KOROMEO KWA KUTUMIA KISU. MWILI WA MAREHEMU
ULIKUTWA KATIKA KIBANDA WALICHOKUWA WANAISHI NA MUME WAKE KATIKA KAMBI
YA UCHIMBAJI MADINI MALI YA ISACK MAMBO. KATIKA TUKIO LA PILI
LILILOTOKEA SIKU HIYO HIYO MAJIRA YA SAA 18:00HRS JIONI HUKO KATIKA
KITONGOJI CHA LONDON WILAYANI CHUNYA MWANAMKE MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA
JINA LA DEFROZA GIDION (18) MKAZI WA KIJIJI CHA ISANZU ALIUAWA KWA
KUPIGWA NGUMI NA MATEKE SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE NA MUME WAKE
ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA JUMA JANUARI. TUKIO HILO LILITOKEA WAKATI
MAREHEMU AKIWA NYUMBANI. VYANZO VYA MAUAJI HAYO NI WIVU WA KIMAPENZI.
WATUHUMIWA WALIKIMBIA MARA BAADA YA TUKIO, JUHUDI ZA KUWATAFUTA
ZINAENDELEA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI
MWANDAMIZI WA POLISI ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI
WALIPO WATUHUMIWA WA MATUKIO HAYO AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI
WAKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE, VINGINEVYO WAJISALIMISHE
WENYEWE.
MWENDESHA PIKIPIKI @ BODABODA AFARIKI DUNIA BAADA YA KUGONGWA NA GARI.
MNAMO
TAREHE 07.02.2014 MAJIRA YA SAA 18:00HRS JIONI HUKO KATIKA ENEO LA
KILIMO UYOLE JIJI NA MKOA WA MBEYA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T.893 BPD
AINA YA ISUZU LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA
LA EMANUEL NSOLO (31) MKAZI WA KIKONDO LILIMGONGA MWENDESHA PIKIPIKI @
BODABODA PIKIPIKI YENYE NAMBA ZA USAJILI T.322 CTJ AINA YA SHINERAY
AITWAYE OSWARD NDUNGURU (26) MKAZI WA IGANZO NA KUSABABISHA KIFO CHAKE
PAPO HAPO NA MAJERUHI KWA ABIRIA WAKE AITWAYE GETRUDA CHARLES MWAKALOBO
(28) MKAZI WA IGANZO. MAJERUHI AMELAZWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA NA
MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALINI HAPO. CHANZO CHA AJALI NI
DEREVA WA GARI KUKATISHA BARABARA BILA KUCHUKUA TAHADHARI. KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI ANATOA WITO
KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA
SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA
KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO
MTUHUMIWA WA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA
SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE, VINGINEVYO AJISALIMISHE MWENYEWE.
WATU WAWILI WAKAMATWA WAKIWA NA NOTI BANDIA MKOANI MBEYA.
WATU
WAWILI WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA PATRICK MSIGWA (34) NA ANTHONY
MWAKIFWAMBA (32) WOTE WAKAZI WA KIJIJI CHA ISYONJE WALIKAMATWA NA
WANANCHI WAKIWA NA NOTI BANDIA 57 @ TSHS 5,000/= SAWA NA TSHS 285,000/=.
TUKIO HILO LILITOKEA MNAMO TAREHE 07.02.2014 MAJIRA YA SAA 15:30HRS
ALASIRI HUKO KATIKA KIJIJI CHA SIMAMBWE WILAYA YA MBEYA VIJIJNI BAADA YA
WATUHUMIWA HAO KUKAMATWA NA WANANCHI WAKATI WAKIWA WANANUNUA CHIPS NA
KUTOA NOTI MOJA YA TSHS 5,000/= NA WALIPOBANWA NDIPO WALIPOONYESHA NOTI
NYINGINE. TARATIBU ZA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI ZINAFANYIKA. KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI ANATOA WITO
KWA WANANCHI KUWA MAKINI WANAPO POKEA/TUMIA NOTI ILI KUEPUKA
KUTAPELIWA.
Signed by:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
No comments:
Post a Comment