Nyama
ya nguruwe. Ugonjwa wa homa ya nguruwe, umeibuka tena katika Jiji la
Mbeya na kuua nguruwe 166 wenye thamani ya Sh33 milioni hadi ilipofika
juzi. Picha na Maktaba
Ugonjwa
wa homa ya nguruwe, umeibuka tena katika Jiji la Mbeya na kuua nguruwe
166 wenye thamani ya Sh33 milioni hadi ilipofika juzi.
Tayari
Mganga Mkuu wa Mifugo katika jijini hilp, Dk James Kawamala ametangaza
karantini ya kuzuia kuingia au kutoa nguruwe kwenda katika eneo lingine.
Kwa
mujibu wa matangazo yaliyobandikwa katika maeneo mbalimbali ya Jiji, ni
marufuku kwa mtu yeyote kuchinja ama kusambaza na hata kutoa zawadi ya
nyama ya nguruwe ambaye haijathibitishwa na daktari wa mifugo wa jiji.
Alipoulizwa kuhusu hali ya ugonjwa huo, mganga huyo alisema ni mbaya na kwamba tayari nguruwe 166 wamekufa hadi juzi.
Alisema taarifa zinasema ugonjwa huo pia umeripotiwa katika Wilaya za Rungwe na Mbeya Vijijini.
‘’Kwa
namna yoyote ile, wanyama wote wa jamii ya nguruwe kwa sasa watatakiwa
kuthibitishwa kwa kuliwa katika machinjio zilizopo jijini hapa,’’
alisema.
Ugonjwa
wa homa ya nguruwe kwa mara ya kwanza ulizuka mkoani Mbeya mwaka 2011
ambapo nguruwe wengi walikufa na watu kupata hasara.
Kwa mujibu wa Dk Kawamala, Jiji la Mbeya, pekee ilipoteza nguruwe zaidi ya 1,500.
MWANANCHI
No comments:
Post a Comment