
Wakizungumza na kituo hiki wakazi wa kijiji hicho wamesema
hali ya usari ni mbaya kutokana na kutegemea gari moja kwa muda mrefu
na kupelekea msongamano mkubwa wa watu .Aidha Bw Marino layachi
ameongezea kuwa pamoja na vyombo hivyo vya usafiri kuwepo ila bado
havikidhi mahitaji kutokukana na kuharibika mara kwa mara.Nae afisa
mtendaji wa kijiji hicho Bw Yohana Mesai
amesema wame fikisha swala hilo sehemu husika lakini hakuna
utekelezaji wowote ulifanyika na hivyo ameitaka
mamlaka ya usafirishaji majini na Nchi kavu (SUMATRA) kuwajali wakazi
wa vijijini .
kwa upande wake Afisa mfawidhi wa mamlaka ya usafirishaji majini na Nchi kavu kanda ya kati Dodoma
Bw Bahati Musiba amesema wao wanatambua safari zinazofanywa kutoka Dodoma mjini kuelekea Izava hivyo
amewataka wamiliki wa vyombo vya usafiri kujitokeza ili wapewe leseni bure za usafirishaji
vijijini.Na dodoma fm
No comments:
Post a Comment