WAZIRI
MKUU Mizengo Pinda, amepokea msaada ya mabati, mashuka, vyandarua na
biskuti vyenye thamani ya sh. 141,045,000/- kutoka kwenye makampuni
binafsi matatu na jumuiya za kidini mbili.
Akizungumza
wakati wa makabidhiano hayo leo Jumatatu Februari 3, 2014 katika Ukumbi
wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Mwenyekiti wa Makampuni ya (MMI) Steel Ltd.
Bw. Subhash Patel alieleza kuwa jumuiya yao imeguswa na tukio hilo na
kuona umuhimu wa kutoa misaada hiyo.
Akikabidhi
misaada hiyo, Bw. Patel alitoa wito kwa makampuni, taasisi za dini na
watu binasi kuchangia waathirika wa mafuriko hayo ili waweze kuendelea
na maisha yao ya kawaida.
Akipokea
misaada hiyo, Waziri Mkuu Pinda alishukuru sana jitihada zilizooneshwa
na kampuni hizo kwa misaada waliyotoa, kwani nyumba, Zahanati na makazi
ya wananchi wengi yaliondoshwa na maji.
Akizungumza
na waandishi wa habari, Waziri Mkuu alisema: “Nilitembelea eneo lile na
kuona kwa jinsi gani maji yalivyoathiri eneo kubwa kwa kuingia ndani ya
makazi ya watu, hali iliyosababisha kupotea kwa mazao, chakula kingi
kilipotea hivyo misaada bado inahitaji kwa wingi kwa wananchi wale”.
Waziri
Mkuu alisema Rais ametoa maagizo kwamba Jeshi lijenge nyumba za muda
ili kuweza kuwahifadhi wananchi wa eneo lile. “Serikali imefanya
jitihada kwa kupeleka mahema, na kuanza ujenzi wa haraka wa daraja ili
kurejesha usafiri katika hali ya kawaida.
Ametoa
wito kwa wananchi na makampuni yanayotaka kuwasilisha misaada yao,
wanaweza kuiwasilisha moja kwa moja kwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro na hapa
Dar es Salaam wanaweza kuiwasilisha katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara
ya Maafa.
No comments:
Post a Comment