Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Saturday, February 8, 2014

Watu tisa watiwa mbaroni kwa tuhuma za mauaji ya wanawake wawili wanaodaiwa kuzuia mvua kunyesha mkoani Simiyu



 
Na Chibura Makorongo, Simiyu.
Jeshi la polisi mkoani Simiyu linawashikilia watu tisa wakiwemo wanawake wawili wa kijiji cha Mwabulimbu wilayani Maswa kwa tuhuma za mauaji ya kikatili ya kina mama wawili kuuawa na kuchomwa moto kwa kudaiwa kuzuia mvua kunyesha.

Mbali  na   wanawake hao polisi pia inawashikilia viongozi wakuu wa jeshi la ulinzi wa jadi "Sungusungu" akiwemo Mtemi  na Kamanda wake mkuu kwa tuhuma za mauji hayo ya kikatili kwa akina mama hao ambao baada ya kushambuliwa sehemu mbalimbali za miili yao walichomwa moto kwa madai ya kuzuia mvua kunyesha katika kijiji cha Mwabulimbu wilayani hapa.
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Simiyu Charles Mkumbo akiongea na waandishi wa habari jana ofisini kwake alisema  kuwa viongozi waliokamatwa ni Mtemi mkuu wa sungusungu Ntalage Mabula (50) na Kamanda wake mkuu Sosoma Mamuda (50) wote wakazi wa kijiji cha Mwabulimbu,kata ya Mwang'honoli tarafa ya Sengerema  wilayani Maswa mkoani hapa. 
Wanawake waliokamatwa kuhusiana na mauaji hayo ni Tabu Mongo (31) na Joyce Kija (30) watuhumiwa wote ni wakazi wa kijiji cha Mwabulimbu kata ya Mwang'honoli  tarafa ya Sengerema wilayani Maswa.
Akielelezea tukio hilo kamanda wa polisi alisema watuhumiwa wote walikamatwa februari 4 kufuatia viongozi hao wakuu wa sungusungu mnamo februari pili mwaka huu,kutoa amri na agizo la kupiga yowe na filimbi za hatari na kukusanya wananchi waliowapiga na kuwaua na kuwachoma moto wanawake hao wawili pia wakazi wa kijiji hicho.
Alisema wananchi hao wakiwa na silaha zao za jadi,marungu,fimbo mawe  waliwauwa wanawake hao na kisha  kuwachoma moto, waliofahamika kwa jina la Gilya Chile (70) na Nyang'au Nyambalya (30) wote wakazi wa kijiji hicho.
Kamanda Mkumbo alisema kuwa kabla ya mauaji hayo, kijiji hicho na maeneo mengine wilayani Maswa na hata mkoa wa Simiyu yalikuwa yakikabiliwa na ukame wa mvua kutonyesha, na inadaiwa kuwa akina mama hao waliomba kuchangiwa gunia moja kila mmoja kwa vile wanatoka katika ukoo wa kichifu ili mvua iweze kunyesha.
Kutokana na kuwepo kwa hali hiyo Mtemi wa sungusungu kwa kushirikiana na Kamanda wake mkuu wa Sunsungu Sosoma Mamuda (50) pia mkazi wa Mwabulimbu walipiga yowe na filimbi za hatari kuhoji kulikoni akina mama hao kuzuia mvua isinyesha kijijini hapo na ndipo walipoanza kuwaadhibu kwa kuwashambulia kwa silaha za jadi.
Kamnda Mkumbo alieleza kuwa watuhumiwa wote hao watafikishwa mahakani mara baada ya upelelezi kumalizika.

No comments:

Post a Comment