Pages

Tuesday, February 18, 2014

WAZIRI MAGUFULI AKAGUA UJENZI WA NYUMBA 851 ZA SERIKALI ZINAZOJENGWA MABWEPANDE JIJINI DAR

Waziri wa Ujenzi,Dkt. John Pombe Magufuli akipata maelezo kutoka Bw. Mwakalinga ambaye ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania.
Waziri wa Ujenzi,Dkt. John Pombe Magufuli leo amefanya ukaguzi wa ujenzi wa nyumba za Serikali zipatazo 851 zilizopo katika eneo la Mabwepande, Kinondoni,jijini Dar es Salaam zinazosimamiwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA). Huu ni muendelezo na mikakati ya Wizara ya Ujenzi ya kuwajengea na kuwauzia watumishi wa Serikali nyumba kwa bei nafuu.

Waziri wa Ujenzi,Dkt. John Magufuli akiendelea na ukaguzi wa Ujenzi huo.
Sehemu ya nyumba hizo.

No comments:

Post a Comment