Pages

Monday, March 31, 2014

AJALI YAUA 22 KIBITI PWANI, YAHUSISHA MAGARI MATANO


Watu 22 wamefariki duniani papo hapo katika ajali ya gari iliyotokea katika kijiji cha Mkupuka tarafa ya Kibiti iliyohusisha magari matano.

Ajali hiyo imetokea jana usiku wa saa mbili kufuatia Hiace iliyokuwa ikijaribu kulipita gari lingine aina ya Tata lenye namba za usajili T 132 AFJ lililokuwa limesimama baada ya kugongana uso kwa uso na gari aina ya Kenta lenye namba za usajili T.774.
Kwa mujibu wa mkuu wa mkoa wa Pwani, Hajjat Mwantum Mahiza, wengi waliokufa ni vijana waliokuwa wanatoka Ikwiriri kwenda Kibiti wakiwa na lori aina ya Fuso na bidhaa zao kwa ajili ya mnada.



 

No comments:

Post a Comment