Pages

Saturday, March 29, 2014

DOCTORS: MATUMIZI YA APP ZA KUCHAT KWENYE SIMU YANAWEZA KUATHIRI AFYA

Daktari mmoja wa Hispania amedai kukutana na mgonjwa wa kwanza wa ‘WhatsAppitis’, tatizo lililotokana na kuchat kwa WhatsApp kwa muda mrefu.
Mgonjwa huyo ambaye hakutajwa jina amedai kupata maumivu katika vifundo vya mkono alipoamka asubuhi.
Baada ya madaktari kumfanyia uchunguzi mgonjwa huyo, walidai kuwa wamegundua tatizo lake limetokana na kuchat kwa masaa sita kwa simu yake kwa kutumia whatsApp.
Dokta Inés Fernandez-Guerrero, wa Granada’s General University hospital amesema kuwa mgonjwa huyo mwenye miaka 34 aliyekuwa na ujauzito wa wiki 27, alianza kusikia maumivu makali katika vifundo vyote vya mikono baada ya kuamka asubuhi.
Baada ya uchunguzi waligundua kuwa mgonjwa huyo hakuwa na historia ya ‘trauma’ na hakuwa ameshiriki katika shughuli yoyote ya kuchosha mwili kupita kiasi katika siku zilizopita, lakini baada ya kuzungumza naye tatizo likajiweka wazi.



Dokta huyo alidai kuwa mgonjwa huyo alitumia simu yake yenye uzito wa g 130 kujibu messages za Whatsapp kwa masaa sita mfululizo.
Mgonjwa huyo alipewa dawa za kupunguza maumivu na kuzuiwa kutumia simu yake.
Madaktari hao wamesema kuwa tatizo kama hilo ni jipya katika matatizo ya hi-tech, na kuwashauri watumiaji wa App za kuchat kama WhatsApp, Viber na zingine kuwa makini wanapochat kwa muda mrefu katika simu zao.

SOURCE: MAIL ONLINE

No comments:

Post a Comment