Machafuko ya hali ya hewa, mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) imetahadharisha
juu ya kuwapo kwa kimbunga kiitwacho Hellen katika mwambao wa Bahari ya
Hindi ambacho kitasababisha mvua kubwa inayozidi mililita 50 ndani ya
saa 24 kuanzia jana katika mikoa 14
Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) imetahadharisha juu ya kuwapo kwa
kimbunga kiitwacho Hellen katika mwambao wa Bahari ya Hindi ambacho
kitasababisha mvua kubwa inayozidi mililita 50 ndani ya saa 24 kuanzia
jana katika mikoa 14.
Taarifa ya mamlaka hiyo ambayo imetolewa jana kwa
vyombo vya habari imebainisha kuwa mvua zitanyesha katika mikoa ya Dar
es Salaam, Mtara, Lindi, Tanga, Unguja, Pemba, Singioda, Dodoma, Ruvuma,
Katavi, Njombe, Mbeya na Morogoro.
Taarifa hiyo imeongeza kuwa mvua hizo zilitarajia
kuanzia jana na zitaendelea hadi Aprili Mosi mwaka huu na wakazi wa
mikoa hiyo, watumiaji wa bahari pamoja na mamlaka zinazohusika na maafa
zimetakiwa kuchukua tahahadhari zinazotakiwa.
Imebainisha kuwa, uwezekano wa mvua hizo ni
asilimia 80 na ni mwendelezo wa mvua za masika zinazoendelea kunyesha
nchi nzima katika baadhi ya maeneo ambako hupata misimu miwili ya mvua
kwa mwaka.
“Mamlaka ya Hali ya Hewa inaendelea kufuatilia na
itatoa taarifa zaidi kadri zitakavyopatikana,” ilisema sehemu ya taarifa
hiyo na kuongeza kuwa, uangalifu na tahadhari vinahitajika ili kuepusha
maafa zaidi.
Kimbunga hicho kinakuja wakati baadhi ya maeneo
nchini, wiki iliyopita zilikumbwa na mafuriko kutokana na mvua
zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali sasa na kusababisha uharibifu
wa mali na miundombinu.
Chanzo;Mwananchi
Chanzo;Mwananchi
No comments:
Post a Comment