1. Je bado inaongelea mambo yaliyopitwa na wakati?
Kama CV yako umeiweka kama ni kitu tu, unatakiwa kuitupa na kuanza upya. CV yako inatakiwa kuwa na nguvu na mwanzo mzuri unaonyesha wewe ni nani kwa maneno unayoanza nayo. CV yako inatakiwa ianze vizuri ili kumvutia mwajiri mtarajiwa, iwe na vitu vitakavyomsaidia kufanya maamuzi ya kukuita kwaajili ya usaili. Watu wengi hawapendi kufanya uchunguzi na kutafuta namna nzuri ya kuandika CV, unafikiri google wapo kwa kazi gani?
2. Je CV yako umeiandika kwa mtindo gani?
Kuna mpango madhubuti kwa kila barua ya kuomba kazi au CV yako. Wewe kama uko viwango vya juu, kama meneja au mkurugenzi na unaandika CV yako kama mtu aliyetoka chuo unaonyesha hauko makini. Vilevile inaweza kuonyesha kwamba huwezi kufanya kazi hiyo na kutia mashaka taaluma yako. Kila kiwango cha elimu na uzoefu kinatofautiana hata namna ya kuandika CV zake, hivyo fanya uchunguzi kujua katika ngazi uliyopo CV ya aina gani inakuwakilsha wewe?
3. Kukosekana kwa Maneno Muhimu
Unapoondoa maneno muhimu kwenye Cv yako, hivyo kama kampuni uliyoomba kazi wanatumia programu za komputa, maneno wanayotaka kwenye CV yako kama hayapo kuna uwezekano mkubwa CV yako kutokusomwa na programu hiyo. Hivyo mwajiri anayetaka kukuajiri anapoangalia CV yako au barua yako kuna maneno anayatafuta kwa haraka kujua kama yapo, kutokuyatumia vivyo hivyo na yeye hatoweza kukuita kwenye usaili.
4. Acha kutumia maneno ya zamani
Jaribu kutotumia maneno ya zamani ambayo yamezoeleka kwenye barua nyingi za kazi, badala ya kusema wewe unaweza kutatua matatizo, elezea matatizo au tatizo ulilowahi kutatua itaonyesha wewe unaweza kutatua matatizo.
5. Kama huelezei ujuzi wako
Kama unataka kushinda au kupata kazi elezea ujuzi wako vizuri na ueleweke. Usitumie kile ambacho watu wote wamezoea kuandika kama ujuzi kumbe ni hulka na tabia. Je ujuzi wako ni nini? Jaribu kujua kazi iliyotangazwa inataka mtu wa aina gani? wenye ujuzi gani?
6. Usiniambie ila nionyeshe
Usipoteze muda kuelezea kitu gani ulikuwa unafanya kama majukumu ya kazi, onyesha umeweza kufanikisha jambo gani kwenye nafasi uliyopo au uliyokuwepo. Napenda kujua ulipata changamoto gani kwenye nafasi uliyokuwapo, je unaelezeaje changamoto hizo na matokeo yake yalikuwa ni nini? Hii inakufanya uwe tofauti na watu wengine, hakuna watu wawili watakuwa na uzoefu wa wa aina moja katika kutatua changamoto, kila mtu atakuja na namna ya tofauti hivyo kukusaidia wewe katiak ushindani kwenye usaili. Tumia hayo kwa faida yako mwenyewe.
7. Kutumia maneno yaliyopoa
Ukitumia maneno yaliyopoa yanaifanya CV yako kuwa ya kawaida sana. Badala ya kusema nilifanya kazi kama……tumia maneno yanayoonyesha kazi zaid ikatika matendo ambayo yatapeleka ujumbe mahili kwa mwajiri huyo. Inamaanisha maneno yanayoonyesha kitu ulichofanya na matokeo yake.
Mwajiri anachoangalia ni matokeo na mafanikio ambayo umeyapata, kama ulizindua mradi au bidhaa, kama uliongoza kufanya kitu fulani, maneno hayo yanamaanisha kitu kwa mwajiri, yanaonyesha kitu kilichofanyika na kuonyesha matokeo ya juhudi ulizochukua.
Vilevile barua yako inatakiwa ionyeshe mambo mawili ya muhimu, Kukamata hisia za anayeisoma ili aisome zaidi na kufuatilia CV yako na kitu cha pili imshawishi kukuita kwaajili ya usaili. Kama Barua na CV yako ni kama vya mtu mwingine yeyote, hivyo hauko kwenye faida ya ushindani na hautaitwa kwaajili ya usaili.
Acha kufanya kama zamani na uonekane kama mtu mwingine, jaribu kuangalia kwa upya nini kifanyike kwenye CV yako na barua yako uonyeshe utofauti.
No comments:
Post a Comment