Pages

Friday, March 28, 2014

Uwanja wa ndege wa Changi wa Singapore washinda tuzo ya uwanja bora duniani 2014, angalia orodha ya viwanja 10 bora zaidi



Uwanja wa ndege wa Changi wa Singapore washinda tuzo ya uwanja bora duniani 2014, angalia orodha ya viwanja 10 bora zaidi
Uwanja wa ndege wa Changi wa Singapore umeibuka kinara na kubeba kwa mara ya pili tuzo ya uwanja bora zaidi wa ndege duniani kati ya viwanja 410 vilivyopigiwa kura na wasafiri zaidi ya milioni 12 na laki 8.
Kwa mujibu wa tovuti maalum ya tuzo hizo zilitolewa jijini Barcelona, Hispania. Mwaka jana uwanja huo ulishinda tuzo hiyo pia.
“Kushinda tuzo hii ya thamani kwa mara ya pili inaonesha kuwa Changi inaonesha kuwa ni zaidi ya uwanja wa ndege.” Amesema Edward Plaisted, CEO wa shirika la Skytrax la Singapore.
Tuzo hiyo hutolewa kwa kukusanya kura za wasafiri wa nchi 110 duniani kote na huzingatia ubora wa uwanja na huduma zinazotolewa kwa wasafiri.


Hiii ni orodha ya viwanja vya ndege kumi bora zaidi kwa mujibu wa tuzo hizo:
  1. Singapore Changi Airport
  2.  Incheon International Airport
  3. Munich Airport
  4. Hong Kong International Airport
  5. Amsterdam Schiphol Airport
  6. Tokyo International Airport Haneda
  7. Beijing Capital International Airport
  8. Zurich Airport
  9. Vancouver International Airport
  10. London Heathrow Airport

No comments:

Post a Comment