Kushuka kiwango
Pamoja
na kufunga mabao 5 katika michezo 12 ya kwanza ya msimu wa EPL, Oscar
ameweza kufunga bao 1 tu katika michezo 14 iliyofuatia na huku kiwango
chake katika eneo la kushambulia kikiwa chini. Takwimu zinaonyesha
kupiga mipira iliyolenga goli kumeshuka kwa 44%. Mchoro wa hapo
unaonyesha takwimu za mchezo wake jinsi zilivyoshuka.
Kama
tunavyoona uwezo wake wa kufunga ulivyoshuka kwa kiasi kikubwa. Kutisha
kwake kwenye kushambulia kumepungua na amekuwa hatengenezi nafasi
nyingi za kufunga pia, amejaribu kutengeneza nafasi 36 katika michezo
26. Willian ambaye amecheza mechi 18 pekee ametengeneza nafasi 39,
wakati Eden Hazard ametengeneza nafasi 77.
Kwa
mchezaji anayecheza kwenye nafasi yake tulitegemea makubwa zaidi, hata
kama Oscar anafanya kazi kubwa bila na mpira katika pressing.
Oscar
hata hivyo anafanya kazi, katika kukaba na kupora mipira. Lakini, Oscar
alishindwa kufanya tackling hata moja dhidi ya Fulham na taratibu
amekuwa akishindwa kulifanyia kazi hili zoezi, ingawa mpaka sasa ameweza
kufanikiwa kwa 59% ya tackling zote alizojaribu.
Nini tatizo?
Tatizo
hili lilianza pale Mourinho alipowaelekeza vijana wake kucheza kwa
kukaba zaidi, Hii ilikuja baada ya michezo kadhaa ambayo Chelsea
walikuwa wakiruhusu magoli mengi na kisha wakapoteza mechi ya Capital
One waliyotolewa na Sunderland. Tangu wakati huo Chelsea wamekuwa
wakicheza kwa kukaba zaidi huku watatu wa kushambulia wakilazimika
kurudi kukaba zaidi..
Oscar
amekuwa akicheza no. 10, Willian kulia pembeni na Hazard kushoto
pembeni, wakati kumekuwepo na mabadilishano, Oscar amekuwa akirudi
kucheza chinizaidi na hivyo kupelekea mchango wake katika kushambulia
uwe mdogo. Dhidi ya Fulham alikuwa akicheza zaidi katika kiungo cha juu,
na sio katika eneo ambalo no. 10 hucheza
Oscar
alicheza chini sana kuliko kawaida. Katika mchezo huu hakufanikiwa
kufanya tackling hata moja, na alijaribu mara tano kufanya hivyo, kitu
ambacho hakiridhishi. Huu ulikuwa mchezo mgumu kwa Oscar, alitengeneza
nafasi moja tu. Mwishowe alitolewa kwenye dakika 77.
Tatizo
jingine ni uchovu. Oscar ni mchezaji ambaye hufanya kazi sana na mfumo
wa Chelsea unamlazimu kucheza kwa namna hiyo. Akirudi nyuma kukaba
pamoja kunyang'anya mipira jambo ambalo linamchosha mno kijana huyo
mwenye miaka 22. Oscar ameshacheza mechi nyingi sana katika misimu
miwili ndani ya Chelsea, mpaka sasa tayari ameshacheza mechi 101, hapo
bila kutaja namba ya michezo ya kimataifa anayoichezea Brazil tangu
ajiunge na Chelsea. Ndio maana haishangazi kuona akiwa amechoka na
Mourinho labda hajampumzisha vya kutosha, hivyo Mourinho anahitaji kumpa
mapumziko kiasi ili aweze kupata matunda mazuri kutoka kwa mchezaji
huyo kwa mara nyingine tena.
Hitimisho
Ni
vizuri kutambua kwamba Oscar ana umri wa miaka 22 na ataendelea kukua
kuimarika kuwa na kiwango kizuri. Amefunga mabao 6 msimu huu, hata kama
hivi sasa anakabiriwa na ukame wa mabao. Msimu uliopita aliweza kufunga
mabao manne tu kwenye ligi hivyo unaweza kuona amefanya vizuri kuliko
msimu uliopita kwenye kufunga. Mfumo wa Mourinho katika kukaba zaidi
unamaanisha Oscar anafanya kazi nyingi zaidi kuliko msimu uliopita,
jambo ambalo linamkaba mwenyewe katika kufanya vizuri kwenye
kushambulia. Anachohitaji sasa ni kufanyiwa rotation na Mourinho na hapo
ndipo tutamuona yule Oscar tuliyemzoea.Na Shaffih Dauda
No comments:
Post a Comment