Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Saturday, March 8, 2014

TAZAMA PICHA::YANGA WAFANYA MAZOEZI USIKU HUU UWANJA WA ALEXANDRIA(MISRI)

Wachezaji wa Young Africans wakiwa mazoezini leo jioni katika Uwanja wa El Max Alexandria
Wawakilishi pekee wa Tanzania kwenye mashindano ya Klabu Bingwa Barani Afrika Young Africans Sports Club leo  usiku wamefanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa El Max Haras El Hodod jijini Alexandria tayari kwa mchezo marudiano kati ya mabingwa watetezi Al Ahly.
Kikosi cha Young Africans kilichowasili mchana wa leo jijni Alexandria kikitokea jijini Cairo kimefanya mazoezi katika uwanja huo utakaotumika kwa ajili ya mchezo wa kesho, huku morali ya wachezaji kuelekea mchezo huo ikiwa ni ya hali ya juu sana.
Wachezaji 20 waliopo Alexandria wamefanya mazoezi chini ya makocha Hans Van der Pluijm, Charles Mkwasa pamoja na kocha wa makipa Juma Pondamali anayewanoa magolikipa na kuhakikisha wanaendelea kuwa fit kwa ajili ya mchezo huo.
Kesho kikosi cha mdachi Hans kitaingia uwanjani kikiwa na kumbukumbu ya ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na Nadir Haroub "Cannavaro" katika mchezo uliofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam na kuhakikisha kinapata ushindi na kusonga mbele katika hatua inayofuata.
Kuelekea mchezo wa kesho ambao utaonyesha na televison zaidi ya 8 za nchini Misri, maandalizi yote yameshakamlika na katika kikao cha maandalizi ya mechi kamisaa ameendelea kusisitiza kuwa mchezo hautakua na mashabiki wa aina yoyote.
Wachezaji waliopo nchini Misri na kufanya mazoezi ya mwisho leo jioni ni"
Magolikipa: All Mustafa "Barthez", Juma Kaseja, Deogratias Munish "Dida"
Walinzi: Juma Abdul, Mbuyu Twite, Oscar Joshua, David Luhende, Kelvin Yondani "Cotton", Nadir Haroub "Cannavaro"
Viungo: Haruna Niyonzima, Saimon Msuva, Athuman Idd "Chuji", Frank Domayo "Chumvi", Nizar Khalfani
Washambuliaji: Mrisho Ngasa, Said Bahanuzi, Emmanuel Okwi, Hamis Kizza, Jerson Tegete na Didier Kavumbagu 
Mechi itachezwa kuanzia majira ya saa 1kamili kwa saa za Misri sawa na saa 2 usiku kwa saa za Afrika Mashariki, na kesho wapenzi, wadau na wanachama wa Young Africans watapatiwa link ya kuweza kutazama mchezo huo moja kwa moja kwa kutumia internet.
Mungu Ibariki Young Africans, Mungu Ibariki Tanzania

No comments:

Post a Comment