CHAMA
cha Wafanyakazi wa Viwanda, Biashara Taasisi za Fedha, Huduma na
Ushauri (TUICO) kimesema wafanyakazi wa Shoprite watalipwa stahili zao
zote Machi 31, mwaka huu. Akizungumza na wafanyakazi wa Shoprite
jijini Dar es Salaam jana, Katibu Msaidizi Sekta ya Biashara TUICO,
Pales Jonathan alisema kuwa, wamezungumza na mwajiri wa Shoprite,
akaahidi atalipa stahili zao zote akishalipa ndiyo ataondoka. Alisema
kuwa, wamekaa kwenye meza ya mazungumzo na mwajiri wa Shoprite, hivyo
hawezi kuuza maduka yake kwa mtu mwingine mpaka atakapomaliza kulipa
madeni ya wafanyakazi. Jonathan aliwataka wafanyakazi wa Shoprite
kuendelea na kazi bila wasiwasi kwani mwajiri mpya ambaye ananunua
maduka hayo NAKUMATT ataajiri wafanyakazi wote wa Shoprite na
atakapoanza wataingia mkataba mpya na ameshakubali. Alisema kuwa
kama bado hawajafikia mwafaka wa kuyakabidhi maduka hayo wataendelea
kufanya kazi kama kawaida na watalipwa mishahara yao na muda wa ziada
baada ya kazi. Hata hivyo alisema, kama kibali cha kukabidhi maduka
hayo hakijatoka kutoka Tume ya Ushindani (FCC) wataendelea kufanya kazi
na watalipwa kwa siku hadi hapo kibali kitatoka.chanzo Majira
No comments:
Post a Comment