Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Monday, April 14, 2014

ALEX MSAMA ANAENDELEA VIZURI BAADA YA KUHAMISHIWA MUHIMBILI

1Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotion ya jijini Dares salaam inayoandaa matamasha ya Pasaka na Krismwass Bw. Alex Msama  anaendelea vizuri baada ya kupata ajali mkoani Dodoma kisha kupelekwa katika hospitali ya mkoa wa Dodoma na baadaye kuhamishiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili katika wodi Kibasila  namba 16 hivi sasa anaendelea vizuri na amesema hali yake imekuwa ikiimarika tofauti na ilivyokuwa Mwanzo, Aliiambia Fullshangwe jana hospitalini hapo kwamba mungu ni mwema na ametenda miujiza yake ndiyo maana amekuwa akiimarika kiafya.(PICHA NA FULLSHANGWEBLOG-MUHIMBILI)
2Mfanyakazi wa Kampuni ya Dira Ally Makuburi akimjulia hali Mkurugenzi wa kampuni hiyo Bw. Alex Msama ambaye amelazwa katika hospitali ya taifa ya Muhimbili, kulia ni Musa Mkama mwandishi wa gazeti hilo pia.3Mfanyakazi wa Kampuni ya Dira Musa Mkama akimjulia hali Mkurugenzi wa kampuni hiyo Bw. Alex Msama ambaye amelazwa katika hospitali ya taifa ya Muhimbili baada ya kupata ajali mkoani Dodoma.5Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akiwa na wafanyakazi wake naa baadhi ya ndugu na jamaa  wakati walipokwenda kumjulia hali katika hospitali ya taifa ya Muhimbili jana.

No comments:

Post a Comment