Bi Habiba Said au Mama Nyamsati aliyejeruhiwa kwa bisibisi na kijana wake wa kumzaa anayefahamika kwa jina moja la Jumanne(28) .
Kisanga! Njemba aliyetajwa kwa jina moja la Jumanne (28), ametiwa mbaroni na polisi Baada ya kumchoma kwa bisibisi mama’ke mzazi aitwaye Habiba Said au Mama Nyamsati na kumsababishia majeraha makubwa kichwani.
kijana Jumanne(28) akitiwa nguvuni.
Ilidaiwa kuwa baada ya wadogo zake
Jumanne kumuona kaka yao akidhamiria kumuumiza mama yao ndipo
wakaingilia kati ili kumzuia, lakini Jumanne aliwapiga wote na kumjeruhi
mdogo wake mwingine kwa bisibisi hiyohiyo.
Raia wakimshangaa kijana Jumanne kwa kitendo alichofanya kwa mama yake mzazi.
Wakati tukio hilo likiendelea,
majirani na ndugu walikwenda kutoa taarifa katika Kituo Kidogo cha
Polisi cha Wailes, Temeke ambapo polisi walifika eneo hilo na kumkamata
Jumanne huku mama yake akipatiwa PF-3 kwa ajili ya matibabu katika
Hospitali ya Temeke. Baadaye mtuhumiwa huyo alihamishiwa Kituo cha
Polisi Chang’ombe.
Ilifahamika kwamba mama huyo alishonwa nyuzi kadhaa kichwani baada ya kujeruhiwa vibaya.
Akizungumza na wanahabari wetu, mama huyo alisema kuwa siyo mara ya kwanza kwa mwanaye kumshambulia kama hivyo kwani aliwahi kumshambulia kwa kumpiga vichwa bila kujali kama alikuwa na mtoto mdogo mgongoni ambaye ni mdogo wake Jumanne.

“Huko nyuma alishawahi kunivamia
nikiwa na huyu mdogo wake mgongoni akanipiga vichwa hadi uso wote
ukavimba,” alisema mama mzazi wa Jumanne na kuongeza:
“Nilisimama naye mahakamani na akafungwa miezi 6 kisha akaachiwa.”
Mzazi huyo alisimulia kwamba chanzo cha mwanaye kuwa katika hali hiyo inawezekana ni mambo ya Kiswahili (kulogwa) kwa sababu siyo kawaida kwa mtoto kumpiga mama’ke.
Mzazi huyo alisimulia kwamba chanzo cha mwanaye kuwa katika hali hiyo inawezekana ni mambo ya Kiswahili (kulogwa) kwa sababu siyo kawaida kwa mtoto kumpiga mama’ke.
Baada
ya soo hilo kufikishwa kituoni hapo, shitaka hilo lilifunguliwa jalada
ya CH/RB/2975/14 KUJERUHI ambapo polisi wanaendelea na uchunguzi ili
jamaa afikishwe mahakamani.
No comments:
Post a Comment