Pages

Tuesday, April 1, 2014

JAPAN YASAIDIA TANZANIA KUINUA KILIMO.

01 (2)Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile (kushoto) akitia saini hati ya makubaliano ya msaada wenye thamani ya ziadi ya bilioni 6 unaolenga kukuza sekta ya kilimo uliotolewa   na Serikali ya Japan  kupitia Shirika la Kimataifa la Japan (JAICA) leo jijini Dar es salaam. Kulia ni Balozi wa Japan nchini Masaki Okanda.02 (2)Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile (kushoto) akikabidilishana nakala ya makubaliano waliosainina na Balozi wa Japan nchini Masaki Okanda (kulia) ambayo yanahusu msaada uliotolewa na Serikali ya Japan  kupitia Shirika la Kimataifa la Japan (JAICA)  jijini Dar es salaam.

……………………………………………………………………….
Na Eleuteri Mangi- MAELEZO
Serikali ya Tanzania imepokea msaada wa zaidi ya sh. bilioni sita (6) za Kitanzania ambazo ni sawa na Yen milioni 380 zilizotolewa na Serikali ya Japan kupitia Shirika lake la Kimataifa la Misaada (JAICA) .
Kauli hiyo ilitolewa  jijini Dar es salaam na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile wakati wa hafla ya kusaini mkataba wa kupokea msaada huo  ambao utatumika kukuza sekta ya kilimo na kupunguza umasikini nchini.

 
Katibu Mkuu Dkt. Likwelile alisema kuwa msaasa huo utatumika kununulia mbolea (UREA) ili kuongeza tija katika uzalishaji mazao na unalenga kuwafikia wakulima wadogo wadogo nchini ili kuwaongezea kipato chao.
Katibu Mkuu huyo alisema kuwa msaada huo umekuja muda muafaka ambapo serikali inachukua hutua za makusudi kuinua sekta ya kilimo ambayo inawaajiri watanzania takribani asilimia 74 nchini.
 Aidha, Katibu Mkuu aliishukuru Serikali ya Japan kwa msaaada huo na kumhakikishia Balozi wa Japan nchini Mh. Masaki Okanda kuwa msaada uliotolewa na Japan kupitia JAICA utatumika kulinganana malengo yaliyokusudiwa.
Kwa upande wake  Balozi wa Japan nchini Masaki Okanda alisema kuwa msaada uliotolewa na Serikali yake kupitia JAICA unalenga zaidi sekta ya kilimo na kusaidia kuimarisha miundo mbinu ya barabara na masoko ambayo ndiyo kiini cha ufanisi katika sekta hiyo.
Naye Mwakilishi wa Mkuu wa JAICA nchini Yasunori Onishi alisema kuwa mahusiano mazuri yaliyopo kati ya Tanzania na Japan ni wa kihistoria ulianzishwa tangu mwakqa 1974 ambapo mkoa wa Kilimanjaro ulikuwa unanufaika na misaada hiyo katika kuboresha kilimo.
Akimshukuru Katibu Mkuu Likwalile na Balozi wa Japan nchini  Okanda, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika Yamungu Kayandabila alisema kuwa amefurahi Wizara yake kupata masaada huo na ameahidi kuwa utatumika kwa malengo yaliyokusudiwa ili kuleta kilimo chenye tija nchini.
Serikali ya Japan nchini kwa kushikiana na Tanzania katika kusimamaia kilimo inaongozwa na nguzo kuu tatu ambazo ni kilimo, miundombinu na utawala bora, hali ambayo itaihakikishia nchi kuwa na uhakika wa mazao bora na hivyo kupunguza umasikini nchini.

No comments:

Post a Comment