Pages

Tuesday, April 1, 2014

MATUMIZI YALIYOKITHIRIKI YA SMARTPHONES YANAWEZA KUHARIBU MACHO

Watengenezaji wa miwani za macho wanahofia kuwa kutazama mwanga unaotoka kwenye vifaa kama simu kunaweza kusababisha matatizo ya muda mrefu ya macho.
Wamedai kuwa watu wanaotumia sana smartphones wanaweza wakawa wanaongeza hatari ya kuharibika macho. Wameonya kuwa utumiaji uliozidi wa simu, kompyuta, tablets na TV za flat screen zinaweza kusababisha madhara hayo.
Mmoja wa watu hao Andy Hepworth alisema mwanga wa blue unaotoka kwenye simu ni hatari kwa macho ya binadamu. Wameshauri kupumzika mara kwa mara kutumia kompyuta ama vifaa vingine vya mkononi.

No comments:

Post a Comment