Safari ya mwisho ya mpendwa wetu Ramadhani Fundikira, (1927-2014). Alifariki tarehe 03/04/2014 saa 10:30 alfajiri katika hospitali ya TMJ iliyopo Mikocheni , Dar es Salaam baada ya kusumbuliwa na figo kwa takriban wiki 3. Leo hii amepumzishwa katika makaburi ya kijijini kwao kaika ikulu ya watemi hao wa ukoo wa akina Fundikira.
Mamia wamehudhuria wakiongozwa na Mh. Samuel Sitta, Aden Rage (Mbunge wa tabora mjini) na viongozi mbalimbali wa serikali mkoani Tabora.
Mazishi yakiendelea eneo la makaburi
Moja ya wajukuu wa marehemu wakirusha mchanga na kumuaaga babu yao.
Kisoma cha mwisho kabla ya mazishi
Mh. Samuel Sitta wakati wakisubiri taratibu mbalimbali kabla ya kisomo na mazishi huko Itetemia
Mmoja ya wajumbe wa bunge la katiba aliyeungana na msafara wa kuuaga mwili wa marehemu
umati wa watu wakiwa eneo la makaburini kwa mazishi
umati wa watu wakiwa eneo la makaburini kwa mazishi
No comments:
Post a Comment