Mike Lukindo enzi ya uhai wake.
Watanzania wa Wisconsin wanapenda kutoa shukurani kwa wote waliojaribu kuokoa kutokuchomwa moto kwa ndugu yetu, mpendwa wetu Mike Lukindo na pamoja na jitihada zote zilizofanyika tunasikitika kuwataarifu kwamba mpendwa wetu ilibidi achomwe moto na jana Ijumaa April 4, 2014 majivu yake walikabidhiwa familia yake kwa mtoto wa kwanza wa marehemu kwenda kuchukua majivu hayo. Mpaka mazishi yafanyike zilikua zinahitajika $6,000 pamoja na michango ya sisi tuliopo Madison, Wisconsin haikuweza kufikia idadi iliyokua inahitajika.
Watanzania wa Wisconsin wanawashukuru vyombo vya habari ndani na nje ya Marekani vilivyosaidia kusambaza habari ya ndugu yetu, mpendwa mwenzetu na Mtanzania mwenzte mpaka habari kuwafikia ndugu zake Tanzania.
Shukurani za pekee kwa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani hususani Mhe. Balozi Liberata Mulamula kwa mchango waliotoa na mara kwa mara Balozi kupiga simu kufuatilia maendelea ya msiba.
Sisi Watanzania wa Wisconsin kwa niaba ya familia tunasema asante na mwenyezi Mungu mwingi wa rehema atawazidishia, Asanteni.
No comments:
Post a Comment