Majeruhi wa awali Joseph Malugu akiwa hospitali ya wilaya ya Kahama baada ya kuumia vibaya mguu wake na sehemu zingine za mwili. |
Msukuma Toroli Fitina Majuto akiwa katika Hospitaliya wilaya ya Kahama
|
Watu
watatu wamelazwa katika hospitali ya wilaya ya Kahama mkoani shinyanga
kufuatia ajali ya kugongwa na gari iliyokuwa ikiendeshwa na mkuu wa
kituo cha polisi cha wilaya ya Kahama Elias Haway huku mmoja akiwa
ameumia vibaya sehemu ya mguu.
Ajali
hiyo imetokea Jana majira ya 1.30 usiku katika barabara itokayo isaka
kuingia kahama mjiniu ambapo Haway akiendesha gari yake Toyota Rav
4 lenye namba T 798 BSK alimgonga mwendesha pikipiki.
Watu
waliogongwa wametambuliwa kwa majina ya Joseph Malugu (35) mkazi wa
Mbulu Bw. Fitina Majuto (20) na Cosmas Peter (21) wote wakazi wa mtaa wa Nyasubi mjini Kahama.
Mashuhuda
wa tukio hilo wamesema Haway alianza kumgonga mwendesha bodaboda Bw.
Malugu katika eneo la Zahanati ya Igalilimi ambapo watu wenye
hasira walimzingira wakimtaka asimame naye akakimbia huku akiwagonga
tena waenda kwa mguu wawili.
Wamesema
Haway alionekana kuwa amelewa hakutaka kuwatii watu waliokuwa
wakimweleza ndipo alipoondoa gari lake kwa mwendo kasi na kwenda
kumgonga Majuto katika eneo la Mkude ambaye aliumia vibaya kwenye
sehemu ya tumbo na kusababisha utumbo kutoka nje.
Wamesema baada ya kuondoa gari eneo Haway hakutaka kusimama na aliendelea na
mwendo kasi ndipo alipokwenda kumgonga mtu mwingine wa tatu Peter
katika barabara ya eneo la Paradise mitaa ya Nyasubi.
Haway
alipohojiwa amekiri kutokea kwa ajali hiyo na kudai kuwa kuna upotoshaji
mkubwa wa taarifa hiyo kwani yeye ndiye aliyegongwa na mwendesha
pikipiki huyo wa kwanza.
Amesema alipotaka kusimama kumwona mtu huyo aliyegonga, aliona watu wameanza kumzonga naye akaamua kukimbia kwa usalama wake ndipo alipoweza kuwagonga tena wale wengine wawili.
Mganga
Mfawidhi wa Hospitali ya wilaya ya Kahama Dk Joseph Foma amethibitisha
kugongwa na gari watu hao na wamelazwa katika wodi namba moja katika
hospital hiyo, huku hali zao zikiwa mbaya na kwamba wapo katika
utaratibu wa kumuhamishia Malugu katika hospitali ya Bugando Jijini
Mwanza.
Via>> Farajimfinanga.info
Via>> Farajimfinanga.info
No comments:
Post a Comment