Maofisa wameelezea kifo cha Warrior kama 'cha kawaida', wakimaanisha hakikusababishwa na matumizi ya dawa za kulevya wala pombe.
Maofisa wamesema ... sababu rasmi ya kifo
cha Warrior, ambaye jina lake halisi ni James Hellwig, kilitajwa kuwa
ni maradhi ya moyo (Atherosclerotic / Arteriosclerotic Cardiovascular
Disease)
Kama
ilivyoripotiwa hapo awali, Warrior alifumbata kifua chake nje ya hoteli
moja iliyoko Arizona Aprili 8, mwaka huu wakati alipokuwa na mkewe
kwenye matembezi ya kawaida.
Alikimbizwa haraka hospitali ya karibu, lakini tangu hapo hakuweza kupata fahamu.
Hadi mauti yalipomfika, Warrior alikuwa na umri wa miaka 54.
No comments:
Post a Comment