Baada ya mlipuko wa bomu kutokea juzi
jijini Arusha, polisi imesihi wananchi kuchukua hadhari, hususan maeneo
yenye mkusanyiko na kutoa taarifa juu ya wanaowahisi mienendo yao si
mizuri.
Aidha polisi imetangaza zawadi ya Sh milioni 10 kwa mtu atakayetoa taarifa juu ya wanaohusika katika kulipua mabomu, ikiwa ni pamoja na waliolipua baa ya Arusha Night Park ya jijini hapa.
Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini (DCI), Isaya Mngulu alikuwa akizungumza na waandishi wa habari jana kuhusu tukio hilo la Jumapili, saa 1:30 usiku eneo la Mianzini kwenye baa hiyo inayomilikiwa na Joseph Kalugendo.
Alisema wataalamu wa mabomu waligundua bomu lingine saa 6:00 usiku kwenye baa iliyo karibu na baa hiyo likiwa ndani ya begi dogo.Uchunguzi wa awali umebaini bomu hilo ni kifaa cha mlipuko wa kutengenezwa kienyeji.
Alisisitiza hadi sasa, hawajakamata mtu yeyote kuhusu tukio hilo huku uchunguzi ukiwa unaendelea.
Alisema majeruhi waliobaki wadini ni wanane na wengine wameruhusiwa. Walio wodini ni Evance Maleko, Evarist Richard, Petro James, Christian Zakaria, Pius Shayo, Antelus Ishengoma, Sudi Ramadhani na Mariam Hans aliyepo hospitali ya Selian.
Alitaka wamiliki wa kumbi za starehe, makanisani, msikitini na maeneo ya mikusanyiko kujitahidi kuweka kifaa cha CCTV kuwezesha kubaini wahalifu.
Kuhusu baa ya Night Park, alisema kwa kuwa kulikuwa na CCTV upo uhakika mhusika atapatikana. Tukio hilo la kupigwa bomu ni la nne jijini hapa. La kwanza ni la Juni mwaka jana katika uwanja wa Soweto. Jingine ni Mei mwaka jana kwenye Kanisa Katoliki Parokia ya Olasiti lililoua watu wanne.
Pia la Shekhe Abdulkareem Jonjo ambaye ni Katibu wa Baraza Kuu la Waislam Tanzania (BAKWATA) aliyejeruhiwa usoni kwa mlipuko wa bomu nyumbani kwake.

No comments:
Post a Comment