Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Friday, April 4, 2014

RAIS KIKWETE AMTEUA MWANDOSYA KUWA MKUU WA CHUO CHA MIST


Rais Jakaya Kikwete amemteua Profesa Mark Mwandosya kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (Mist) wakati Profesa Joseph Msambichaka akiteuliwa Makamu Mkuu wa chuo hicho. 


Katika uteuzi huo uliofanyika mwishoni mwa Machi mwaka huu, Rais pia amemteua Profesa Osmund Kaunde kuwa Naibu mkuu wa chuo upande wa taaluma, utafiti na ushauri, wakati Profesa Emmanuel Luoga ameteuliwa kuwa Naibu Mkuu wa chuo atakayeshughulikia utawala, fedha na mipango.





Taarifa iliyotolewa jana na chuo hicho ilisema kuteuliwa kwa viongozi hao kunalenga kukiimarisha zaidi chuo ambacho kilipanda hadhi ya kuwa chuo kikuu tangu mwaka 2012.
BOFYA HAPA NA ULIKE PAGE YETU KWA HABARI NYINGI

No comments:

Post a Comment