Kutokana
na mvua zinazonyesha hivi sasa kwenye jiji la Dar es salaam pamoja na
kusababisha mambo mengi kusimama, miundombinu kuharibika hasa madaraja
yanayounganisha njia kuu, pia zimesababisha vifo vya watu 10.Nyumba
nyingi zimeingia maji hasa maeneo ya mabondeni na kulazimisha familia
kuhama kutoka kwenye makazi yao ambapo mpaka sasa Polisi Dar es salaam
inasema watu kumi waliofariki, wamo watoto watano na watu wazima
watano.
Kamanda
Suleiman Kova wa kanda maalum ya Dar es salaam amesisitiza hali sio
nzuri hivyo wananchi wanatakiwa wachuke tahadhari kwenye makazi yao na
hata wanaotembea na magari barabarani kwa sababu njia nyingi zina
mashimo na pia watu wapunguze mizunguko isiyo lazima barabarani.Hizi ni baadhi ya picha kati ya nyingi zinazosambaa kwenye mtandao.
No comments:
Post a Comment