TAZAMA PICHA ZA MAMBA ALIYEKAMATWA ZIWA VICTORIA ANA UMRI WA MIAKA 80
Mamba aliekua akiishi katika ziwa
Victoria mwenye umri wa miaka 80, mwenye uzito unaokadiriwa kukaribia
tani moja amekamatwa katika ziwa Victoria upande wa Uganda ni baada ya
wananchi kulalamika kuhusu mamba huyo anaekula watu, huku akikadiriwa
kuwa ameshakula watu wasiopungua sita mpaka kukamatwa kwake
watu wengi kutoka kijiji cha kakira
walifika kushuhudia mamba huyo akitolewa majini, huku wakiwa na nyuso za
furaha na wengi wakipiga picha
Mtu wa mwisho kuliwa na mamba huyo ni mzee mwenye
watoto wawili ambae ni mvuvi wa samaki ambae nguo zake zilionekana
zikielea katika mto huo huko Uganda.
No comments:
Post a Comment