Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akibofya kitufe kuzindua rasmi mpango wa
bima ya afya na maafa wa WESTADI wa mfuko wa Jamii wa NSSF jijini
London, akiwa na Mkurugenzi wa NSSF Dkt RAmadhani Dau na Mwenyekiti wa
Bodi ya Wakurugenzi ya mfuko huo Bw. Abubakar Rajabu (kushoto) . Mwenye
miwani kati ni Bw. Aboubakar Faraji aliyekuwa mwongoza sherehe wa siku
hiyo ambapo Dkt Kikwete alikutana na kuzungumza na Watanzania waishio
Uingereza.
Rais
Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje wa
Uingereza Bw. Hague alipomtembelea ofisini kwake jijini London kwa
mazungumzo Machi 31, 2014 Rais
Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Waziri Mkuu wa Uingereza Bw.
David Cameron alipomtembelea ofisini kwake 10 Downing Street jijini
London kwa mazungumzo Machi 31, 2014
Rais
Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akikaribishwa na Duke of York ambaye pia ni
Balozi wa Biashara wa Serikali ya Uingereza HRH Prince Andrew katika
kasri ya Malkia ya Uingereza ya Buckingham Palace jijini London Machi
31, 2014
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na mwenyeji wake
Waziri Mkuu wa Uingereza Bw. David Cameron alipomtembelea ofisini kwake
10 Downing Street jijini London kwa mazungumzo Machi 31, 2014
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Meya wa Jiji la London
Mstahiki Alderman Fiona Woolf alipomtembelea ofisini kwake Mansion House
jijini London Machi 31, 201
Rais
Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wafanyabishara wakubwa na
wawekezaji wa Uingereza aliokutana nao katika mkutano wa biashara na
uwekezaji katika makao makuu ya Wizara ya Mambo ya Nje na Jumuiya ya
Madola jijini London Machi 31, 2014
Rais
Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wadau mbalimbali wa biashara na
uchumi wa Uingereza aliokutana nao katika ukumbi wa Chatham House
jijini London Machi 31, 2014
PICHA NA IKULU
………………………………………………………………………
Uingereza inajivunia
kuwa nchi inayoongoza katika uwekezaji nchini Tanzania na itaendelea
kuisaidia Tanzania katika jitihada zake za kiuchumi na kuleta maendeleo .
Waziri Mkuu wa Uingereza David
Cameron amemuambia Rais Kikwete wakati wa mazungumzo yaliyofanyika 10
Downing Street, Leo tarehe 31 March, 14, ambapo ndipo yalipo Makao
Makuu ya Waziri Mkuu wa Uingereza.
“Tunafurahia sana uhusiano wetu na kujivunia kuwa tunaongoza katika
Uwekezaji nchini Tanzania” Bw. Cameron amesema na kumhakikishia Rais Kikwete kuwa Uingereza iko tayari kutoa misaada zaidi.
Uwekezaji nchini Tanzania” Bw. Cameron amesema na kumhakikishia Rais Kikwete kuwa Uingereza iko tayari kutoa misaada zaidi.
Rais Kikwete amewasili nchini
Uingereza tarehe 30 Machi, 2014 kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku 3
kufuatia mualiko wa Bw. Cameroon ambaye pia amemuomba Rais Kikwete
aendelee kutoa mchango wake wa mawazo katika masuala ya kimataifa hasa
baada ya mwisho wa muda wa malengo ya millennium ya 2015.
“Tunakaribia mwisho wa muda wa
malengo ya millennia Mwaka 2015, tutahitaji kuweka vipaumbele vingine
baada ya hivyo kama kuondosha umaskini, Maji safi na salama, masuala ya
ufisadi na utawala bora, natumaini utaendelea kutoa mchango wako baada
ya malengo hayo kufikia tamati” Waziri Mkuu Cameron amemuambia Rais Kikwete ambapo Rais amekubali ombi hilo na kuahidi ushirikiano wake.
Mapema leo asubuhi Rais amekutana
na mtoto wa Mfalme Prince Andrew katika makazi ya Malkia ya Buckingham
ambapo wamebadilishana mawazo kuhusu mambo mbalimbali ya Kimataifa na
Kijamii.
Kabla ya kwenda Buckingham Rais
amefungua mkutano kuhusu uwekezaji na kuelezea fursa na nafasi zilizopo
za uwekezaji nchini Tanzania na kuelezea kwanini wawekezaji watakuwa
wanafanya uamuzi bora kwa kuwekeza Tanzania kuwa ni pamoja na;
“Fursa nyingi, amani, usalama, soko la kutosha na kubwa kwa vile Tanzania iko katika Umoja wa Afrika Mashariki, Ukanda wa Maziwa Makuu na Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika,hivyo kuwa na uhakika wa soko kubwa na pana” amesema.
“Fursa nyingi, amani, usalama, soko la kutosha na kubwa kwa vile Tanzania iko katika Umoja wa Afrika Mashariki, Ukanda wa Maziwa Makuu na Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika,hivyo kuwa na uhakika wa soko kubwa na pana” amesema.
Katika ziara yake Rais pia
amekutana na Mstahiki Meya wa Jiji la London Mama Alderman Fiona Woolf
na kukaribishwa rasmi Jijini London. Mstahiki Meya anatarajia
kutembelea Tanzania, Mwezi Septemba Mwaka huu.
Rais alipowasili London tarehe 30
Machi,2014, alikutana na Watanzania wanaoishi nchini Uingereza na
kuwaeleza maendeleo yaliyopo nchini Tanzania.
Rais anaendelea na ziara yake nchini Uingereza
Mwisho.
Imetolewa na;
Premi Kibanga.
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
London Uingereza
31 Machi, 14
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
London Uingereza
31 Machi, 14
No comments:
Post a Comment