skip to main |
skip to sidebar
YALIYOTOKEA LEO ASUBUHI KWENYE BUNGE MAALUMU LA KATIBA HAYA HAPA
Kikao cha bunge maalum la katiba kimeendelea leo hii, kinachojadiliwa hasa ni sura ya kwanza na sita ya kwenye rasimu ya katiba.
Mh. Mbarouk anaunga muundo wa serikali mbili maana ndo anaamini utawapa Zanzibar utajiri na Zanzibar itakuwa half London.
Mh. Hija Hassan Hija anasema watanganyika hawana hasara ya
serikali mbili wala moja maana walishachukua mali zote kwa miaka hamsini
iliyopita na Zanzibar wameibiwa kwa miaka hamsini iliyopita.Zanzibar
ilipwe fidia ya miaka hamsini iliyopita.
- Anasema wenye mali ni Tanganyika,mawaziri wa Zanzibar wamekuwa
wakisema muungano umekuwa ukiwaonea na anashangaa ni nini
kimewapata.Anasema kuna mawaziri wana maslahi yao ndo maana wanashindwa
kuipigania Zanzibar.
- Anasema mawaziri hawatetei muungano bali wanatetea maslahi yao maana
kuna watu walikuwa wanapigania muungano ila baada ya kupewa uwaziri
wakakaa kimya kwahiyo hawa ni wasaka tonge wana njaa.
Mh. Silima anasema yeye ni muumini wa muundo wa serikali
mbili.Anasema mfumo huu umesaidia katika nyanja mbalimbali katika kuleta
amani,nguvu na mshikamano Tanzania.
- Hakubaliani na muundo wa serikali tatu kutokana na hofu anayoiona
mbele.Anaogopa kusikia kuwa kuna serikali ya Zanzibar,Tanganyika pamoja
na ya Muungano.
- Anawaomba wabunge wasiruhusu kuupa mwanya muundo wa serikali tatu ili kuleta amani na kudumisha utaifa uliopo.
- Anasema ni muumini wa serikali mbili zitakazofanyiwa marekebisho ili kutoa changamoto zilizopo sasa.
-Asema muundo wa serikali tatu utaleta gharama kama kutakuwa na marais watatu,mahakama za serikali tatu
Mh. Felisia .Anaipongeza tume kwa kazi waliyoifanya kwa kuandika sura zote za rasimu ya katiba mpya.
- Anasema yeye ni muumini wa serikali inayoleta umoja na mshikamano ambao ni tofauti na nchi nyingine ambao ni serikali mbili.
- Hataki kuona mzanzibar na mtanzania bara wakitengana kwa mambo yasiyo na msingi.
Mh. Mbarouk Ally - Anaunga mkono taarifa ya wachache ya kamati namba nne na marekebisho yote waliyofanya.
- Anasema Muundo wa kuwatoa kwenye matatizo yaliyopo ni muundo wa shirikisho wa serikali tatu.
-Anasema wazanzibar wamechoshwa na muundo huu wa serikali mbili na
anasema hakuna mzanzibar ambaye anataka muundow huu uliopo maana umekuwa
kero sana kwao.
-Anasema Miaka hamsini wanazungumzia kero hizi za serikali mbili naa
badala ya kupungua zinaendelea kuongezeka.Anasema kamati na tume
mbalimbali zimeundwa kutatua migogoro mbali mbali za muungano na bado
zimeshindwa na nyingnie zilikuwa chini ya waziri mkuu wa muungano na
viongozi wengine na bado zimeshindwa.
- Anasema wazanzibar wamechoshwa na udharimu wa muundo wa serikali mbili.
- Anawaumbua viongozi wa zanzibar wakija Tanzania bara wanaunga muundo
wa serikali mbili lakini wakirudi zanzibar wanaanza kulilia muundo wa
serikali tatu.Anasema wazanzibar wasipokuwa makini hata vyeti vya ndoa
vitatoka Dodoma.
Mh. Pamela Masai - Anasema wajumbe wameacha maslahi yenye tija kwa watanzania na wote na kukimbilia kwenye muundo wa serikali.
- Anaunga mkono maoni ya wachache kwenye Kamati namba 10.Na anaunga mkono Lugha ya kiswahili kutumika kama lugha ya taifa.
- Anapinga vipengele vya Uadilifu,uwajibikaji uwazi na usawa kuondoshwa kweye tunu ya taifa.
-Anasema kamati zote zimeunga mkono sura ya pili ibara ya sita 2(6)
,anasema kwahiyo hata mamlaka waliyonayo wajumbe wa BMK ni mamlaka
waliyopewa wananchi.
- Anapendekeza muundo wa Serikali tatu.Anasema kama wananchi wanataka
serikali mbili basi waendelee na serikali tatu alafu wananchi
wapendekeze maoni ya muundo wa serikali wanayotaka.
Mh. Mwinyi Haji Makame - Anasema muungano huu waasisi wetu wameleta muungano wa undugu na sio vinginevyo.
- Gari ya serikali mbili ishachemka na haizuiliki,anasema hata wakina
Jussa wakileta unafiki na chuki muundo huu utaendelea kuwepo..
-Anasema miaka hamsini ya mapinduzi ndio umeijenga Zanzibar.
- Anamalizia kwa kusema kuwa matatizo ya Zanzibar kwa muundo huu wa
serikali mbili yashashughulikiwa ndani ya kamati zote zilizoundwa
kutatua matatizo ya wazanzibar.
Mh. Asumpta Mshama - Anaanza kwa kuelezea kinga ya bunge. Anasema wananchi ndo watajua na kupima yapi ya kweli baina ya wale wanayozungumza wabunge ili waweze kuamua.
- Anasema rasimu imeleta serikali tatu lakini walio wengi wamesema
wanataka serikali mbili.Anaiponda tume ya Warioba kuwa pamoja na usomi
wao kwa hili la kuleta serikali tatu haoni mantiki ya usomi wao na
anasema anaona kama hawajasoma kabisa.
- Anasema watu waokaa na kuandaa maangamizi kamwe hawawezi kuwa wasomi kabisa.
- Anasema utamuduni wetu ni muundo wa serikali mbili na hawawezi
kuchomoka kabisa na ansema ili serikali tatu iwepo lazima kwanza muundo
uliopo uvunjwe na hayupo tayari kuona hilo jambo likitokea na hakuna wa
kutenganisha mchanga wa Zanzibar na Tanganyika na anasema muundo wa
serikali tatu ni mzigo kwa wananchi maana kodi ya watanzania itapotea
bila sababu za msingi.
Mh. Chiku Abwao - Anaanza kwa kusema yeye ni muumini wa muungano
na muungano wa shirikisho ndo utaondoa muungano wa manung'uniko na
kuhakikisha Tanganyika inapatikana kwa ghalama yoyote, ananukuu ''Jasiri
ni yule anayejali kwao''
-Anasema bora muungano uvunjike ila Tanganyika ibaki na anaunga muundo
uliopendekezwa na tume ya Warioba maana ni maoni ya wananchi walio
wengi.
- Anamnukuu Lukuvi kuhusu jeshi kutawala nchi kama muundo wa serikali
tatu ukipita na kusema hata hivyo jeshi lipo kwa ajili ya wananchi wa
Tanzania pia anawasifu wazanzibar kwa kupigania utaifa wao.
- Anasema wabunge walio wengi wa tanzania hawapo bungeni kuunga muungano
wa tanganyika na zanzibar bali wapo kuunga mkono muungano wa TANU na
AFRO-SHIRAZI Party.
- Mh. Anaunga mkono kamati yake no saba na waliofanya marekebisho
sura 1&6 kwa muundo wa serikali 2 na anawaunga mkono wananchi wengi
waliokubaliana na muundo wa serikali mbili.
- Analaani kitendo cha mh. Hija kwa kitendo chake cha kutukana mwanamke maana naye kazaliwa na mwanamke.
- Anasema wapemba wameanza ubaguzi baada sherif Hamad kuukosa urais na
anamtuhumu mh sherif Hamad kuwa muasisi wa ubaguzi wa kipemba na
kingazija.
- Anataka hati ya muungano wa pemba na unguja iletwe bungeni na ioneshwe
kwa wajumbe.Anasema viongozi CUF Zanzibar ndio wanaotaka kuuvunja
muungano na sio wazanzibar wote.
Mh. Oluoch - Anasema kumbe bungeni ni sehemu ambapo ukweli
unaachwa na uongo kuchukuliwa. Anasema hata waasisi waliunganisha
mchanga wa Tanganyika na Zanzibar ili kuunda serikali moja na sio mbili
kama ilivyo sasa.
- Anasema ikiwa wazanzibar wakitaka muungano hawatapika kura ya kuunga muundo wa serikali mbili...
- Anasema walimu wanaunga hoja serikali tatu.
Shamsa Mwangunga - Anatoa pongezi kwa serikali ya JMT kwa kulea muungano huu mpaka kufikia miaka 50 maana malezi yanapitia changamoto nyingi.
- Anasema muungano huu ni tunu maana nchi nyingi zimejaribu kuwa na
muungano na shirikisho ila hawakuweza kufika mbali ila kwa muungano huu
wa tanzania ni swala la kujivunia kuwepo mpaka sasa hivi. Uvumilivu na
upendo wa watanzania ndo umeleta muungano huu kuwa imara na kero mbali
mbali zimeweza kutattuliwa na kubaki kero moja ya uchumi.
- Utawala bora tumekuwa tukisifiwa duniani kwa kuwa na utawala bora kwa
kuweza kuudumisha muungano huu na kuna watu wamekuwa wakipotosha kuwa
kuna kero wakati sio kweli hakuna kero na kero zilizobaki ni ndogo na
zinafanyiwa kazi.
Anasema serikali ya nchi mbili ni zimwi tulijualo na tumelizoe na
serikali ya nchi tatu hatulijui ''Zimwi likujualo halikuli
likakwishaaaa''
Mh. Salehe Nassoro Juma - Anaelezea msimamo wake ni muungano wa
serikali tatu na anawatoa wasiwasi watanzania na wapemba wanaofanya
biashara ya vitunguu tanzania bara kuwa serikali tatu hazivunji muungano
na kama ukivunjika tanzania imeasini mkataka wa haki za binadamu na
wataendelea kuishi kama DIASPORA hata muungano ukivunjika.
- Anamshukuru mh. Kikwete kwa kuanzisha mchakato huu wa katiba
mpya,maana kabla ya mchakato huu ilikuwa kosa la jinai kuzungumzia
muundo wa muungano.
-Anasema hakuna asiyejua kuwa muundo wa serikali mbili una tatizo na
suluhisho la matatizo haya ni muundo wa serikali tatu,anasema pia kuwa
mawazo ya waasisi wetu yamezeeka inabidi yafanyiwe modification na
ametolea mfano wa China jinsi walivyofanyia modification mawazo ya
waasisi wao na mambo yanaenda vizuri.
Mh. Haji Omar - Anaanza kwa kuunga mawazo aliyoyatoa kwenye
kamati no 7 mawazo ya walio wengi kwenye sura ya 1 & 6 juu ya muundo
wa serikali mbili.
- Uhalai wa Karume kuchukua dhamana ya watu wa zanzibar kuhusu
muungano,anasema mzee Karume alikuwa anatimiza ilani ya chama chake cha
ASP juu ya umoja na kuhakikisha elimu inakuwa bure,matibabu bure,makazi
bora kwa wazanzibar wote.
Faida za muungano, anasema
1.Umeme jimbo la Tumbatu
2.
-Anasema wananchi walio wengi Zanzibar wanaunga muundo wa serikali mbili
Mh. Panya Abdallah - anaunga mapendekezo ya wengi kutaka serikali mbili iendelee.
- Anawapongeza waasisi wetu kuweza kuunda muungano huu na maadui wengi
wameshindwa kuuvunja na wataendeleza yale yote waliyoyaacha.
- Anasema muungano hauwezi kuvunjwa kwasababu ya kero wako kero ni jambo linaloweza kufanyiwa kazi na kutekelezeka.
- Anasema kuwa CUF wanataka serikali tatu na CCM wanataka serikali mbili
na CUF ndani ya Zanzibar wanasema wanataka serikali ya ''M(N)KATABA''.
- Anasema CUF hawautaki muungano ila njia nyepesi ya kurudi mkoloni.
Mh. Ezekiel Maige anasema kuwa lugha zinazotolewa na Wazanzibari
zina ukakasi. Anasema kuwa Zanzibar ina wilaya 10 ambazo zote zina
barabara za lami na umeme tofauti na Tanzania Bara.
- Anasema kuwa hayo yote hawayaoni na badala yake wanazidi kulalamika
kuwa wanaonewa na Bara. Anahoji iwapo ikatokea Zanzibar kukawa na
utajiri Mkubwa kuliko Bara, je Wazanzibari watakuwa tayari kuisaidia
Bara.
Mh. Fahmi Dovutwa anasema, Alama za taifa zitakua Wimbo wa taifa,
nembo ya taifa na bendera. Dora haimtambui Mungu kwa hiyo iyo wimbo wa
taifa itolewe kwenye alama ya taifa. dhana ya Kuomba Mungu asaidie
inamaana Dola inasilikiliza wanaMungu tu wakati taifa hili
halifungamani na dini. Nami ntasimama ntapigana kuhakikisha Katiba
inamtambua Mungu.
- Kuzuia mtu kumnyonya mtu mwingine. Sera ya TANU iliruhusu wazee watoto
na walemavu kunyonya. nataka iwe kutegemeana sio kunyonyana.
- Watu wanaoamini serikali tatu mpaka sasa wameshindwa kutuonesha jinsi
watakavyo tatua matatizo tulio nayo. watu wa serikali tatu wameshindwa
kujenga hoja. Namlaumu sana Mbowe. Chadema wana wana serikali za
majimbo lakini wanashindwa kufafanua vizuri.
- Natoa shukrani za pekee za rais kwa kuridhia hii ijadiliwe na
kusimamia elimu za kata. namshukuru pia Lowasa aliye mshauri Rais.
Mh. Joseph Mbilinyi anasema: Naunga mkono serikali tatu kama ilivyoletwa na Tume ya katiba,kwa hiyo tunaunga mkono maoni ya wananchi.
- Aliye haribu huu mchakato ni Rais aliyekuja kuelezea msimamo wa chama chake badala ya kuzindua bunge.
Hiki ni kipindi cha kwaresma acheni unafiki. Tumeharibu pesa nyingi. CCM
wameishiwa mikakati wameanzisha mkakati wa kuzomea. Mwingulu anataka
serikali moja lakini anaogopa kusema. Tuko kwenye nafasi nzuri sana la
kujadili hili swala la sivyo tutalijadili kwa kulazimishwa.
- Leo Lukuvi anatutishia nchi itatawaliwa na jeshi vizuri,mbona rais
wetu alikua mwanajeshi na anatuongoza? wanajeshi ni ndugu zetu,
wakitawala kuna tatizo gani?
- Serikali tatu ni tija. kila chenye gharama kina faida. Mara nyingi
viongozi wa dini wanakosea wanapokuwa upande wa dola dhidi ya wananchi.
Mfano Rwanda. Unapopima maralia au ukimwi inapimwa kwenye kidole sio
mwili mzima acheni kuzingua eti walio hojiwa ni wachache.
Mh. Mahamood Mussa anasema, Naomba Muongozo wako. Humu ndani ulituambia anakuja Rais au mwenyekiti wa CCM?.
- Katika kamati yetu baadhi ya wajumbe walikua wanazungumzia sikukuu za
kitaifa upande wa zanzibar. wenye walikua wanatambua 10/12. wenzetu
wanakubaliana na katiba ya 63 ya mkoloni.
- Walitudanganya wamepita kutafuta hati za Muungano hadi un hawakuzipata
wakati zipo dar. sasa zimepatikana, wataongea nini tena?
- Tuliungana kuunganisha ulinzi, kutumia soko na ardhi ya Tanganyika.
haya ndo yalikua malengo ya muungano. Tunaendeleza serikali mbili
asanteni sana.
Mh. Pindi Chana, Anaanza kwa kuunga mkono serikali mbili.
- Anasema haiwezi ikawa nchi na shirikisho lazima tuchague moja ama
nchi ama shirikisho. Iwe serikali mbili kwa sababu imetokana na hati ya
makubaliano.
- Anauliza serikali tatu imetokana na chimbuko la hati ipi?
- Wananchi wananiuliza hivi hayo Marais watatu watalipwa na nini? je
wataishi wapi au hapa Ludewa. Walimu wana vipaumbele vyao sio serikali
tatu..
- Serikali wanazozitaka watanzania ni serikali mbili. hata humu ndani
watu wengi wanaochangia wanataka serikali mbili. Hiyo serikali yenu ya
tatu haina bunge, mahakama wala visa.
- China nchi ni kubwa lakini ina rais moja. USA kubwa lakini ina rais
mmoja sisi eti marais watatu, watanzania tuwe makini sana.
- Namshukuru Balozi Ombeni Sefue kwa kutuonesha hati ya makubaliano.
- Kabla ya 1992 tulikua na chama kimoja CCM,kulikuwa na document za kidumu chama cha mapinduzi.
- Serikali mbili hazikwepeki, kama tukitaka kutest tusitest kwa watanzania.
Mh. Jesca Msambatavwangu,anaanza kuzungumzia kero za muungano,
- Ibara 34(1) ya katiba ya JMT, inaonesha Tanzania Bara imechukua sehemu
kubwa ya muungano,anasemna hayo yalikuwa mawazo ya waasisi wetu.
- Malalamiko yaliyo mengi ni kwamba tumechukua mambo ya muungano na
tumeyachukua kuwa ya kwetu ndo maana Zanzibar wanalalamika. Sasa
tuandike katiba mpya kwa upendo na hekima.
- Orodha ya mambo ya muungano iliyo elezwa wakati wa muungano
yanaendelea kuongezeka kila siku. Tuache kuongea maneno ya wanaume
waliyo tangulia bali tuongee maneno yetu sio fulani alisema hivi.
- Kama tunasema orodha ya muungano yatakua saba tupange sisi hakika tutaridhiana.
- Mimi naunga mkono serikali mbili lakini inaonekana tumeimeza Zanzibar.
- Mimi naomba swala la muundo Rais wa Zanzibar abaki kuwa ni makamu wa
rais wa Muungano na rais wa muungano aendelee kuwa rais wa Tanzania
bara.
- Zikiwa serikali tatu halafu hizo serikali tatu zikazembea kuwalisha haya majeshi ya serikali tatu haya majeshi yatatugeuka.
- Hoja ya gharama. Unaposema serikali ya tatu haina gharama ni uongo usiopingika.
- Hati ya muungano. ukiona mtu anazungumzia maswali ya hati ya ndoa jua
kuna mawili ama kapata mtu mwingine au anataka kwenda mahakamani
kuvunja ndoa, muogope sana.
Mh. Abdallah anasema, Mimi na wananchi wangu tunaunga mkono
serikali tatu. Lengo kuu ni kuondosha utata uliopo wa kikatiba. Msomaji
wa maoni ya walio wengi alisema;
- Marekebisho ya walio wengi yakipita Zanzibar itabidi irekebishe katiba yake.
- Nilivyosikia hivyo nikaogopa,nikajiuliza kama hoja hiyo ikienda kwa wananchi ili mipigiwe kura watakataa?
- Wanasema Zanzibar imeruhusiwa kujiunga na OIC ni uongo. Sisi ndugu
zenu mbona hatujui? Hadi leo hakuna fedha iliyopatikana toka Zanzibar
kwenda benki kuu.
- Njia pekee ya kuondokana na hili tatizo ni muundo wa serikali tatu,
hizi pesa za Zanzibar kila siku wanakokotoa zimekua kokoto hadi
zisiletwe?
- Zimekuwa kama Balali au ndege ya Malaysia hazionekani?
==============
Mwenyekiti wa BMK anasema muda umeisha na hata kama wakimpa nafasi mjumbe anayefuata kuongea muda hautatosha.
Anaanza kusoma matangazo na anatangaza kamati ambazo zitakuwa na vikao jioni.
Anatangaza baadhi ya wageni wa wajumbe wa bunge maalam la katiba na wageni wengine waalikwa.
Anamkaribisha waziri wa katiba na sheria wa SMZ kutoa muongozo wa
kuahirisha bunge maalum la katiba kabla ya muda ili waweze kujiandaa na
vikao vya jioni.
Walioafiki wameshinda na mwenyekiti kwa utani anasema ''Ambao hawajaafiki basi wabaki ndani ya bunge''.
Mwenyekiti anaahirisha BMK mpaka leo saa 10 jioni.
No comments:
Post a Comment