Guinness World Records wamethibitisha kuwa Dr. Alexander Imich wa mjini New York ndio mwanaume aliyehai mwenye miaka mingi zaidi duniani. Dr Imich anamiaka 111.
Dr. Imich amezaliwa February 4th, 1903. Mwaka 1951, Imich na mke wake walihamia Marekani kutokea Soviet Union na kuishi Manhattan akiwa mwenyewe toka mke wake afariki mwaka 1986.
Aliyekuwa akishikilia rekodi hii amefariki ni Arturo Licta wa italia, alifariki April 24th akiwa na miaka 111 na siku 357.
Misao Okawa wa Japan mwenye miaka 116 yupo kwenye rekodi ya Guinness kama binadamu aliyeishi miaka mingi zaidi duniani. Alizaliwa March 5, 1898 na anaishi Osaka.
Fahamu binadamu aliyewahi kuishi miaka mingi zaidi na kuweka rekodi liishi miaka 122 na siku 164. Alikuwa Jeanne Louise Calment wa Ufaransa.
credit : sam misago
No comments:
Post a Comment