Pages
▼
Thursday, May 8, 2014
Deni la Taifa limepanda kutoka trilioni 16.98 cha mwaka wa fedha 2011/2012 hadi kufikia trilioni 21.2 kiwango ambacho kikigawanywa kwa kila Mtanzania kila mmoja atatakiwa kulipa Sh. 471,111.
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh, ameweka hadharani deni hilo wakati akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari mjini Dodoma juu ya ripoti ya ukaguzi kwa mwaka wa fedha 2012/13 iliyowasilishwa bungeni.
Utouh amesema ongezeko hilo limesababishwa na mikopo kutoka kwenye mabenki na nchi wafadhili kwa ajili ya kusaidia miradi mikubwa ya maendeleo.
Utouh amesema deni la nje limefikia Sh. trilioni 15 hadi Juni 30, 2013 ambalo ni ongezeko la Sh. trilioni 3.0 kutoka Sh. trilioni 12.43 kwa mwaka 2011/12, wakati lile la ndani limefikia Sh. trilioni 5.78 ikiwa ni ongezeko la Sh. trilioni 1.23 kutoka Sh. trilioni 4.55 kwa mwaka 2011/12.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Zitto Kabwe, amepongeza ukaguzi huo kubaini mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kunusuru fedha za walipakodi ambapo amesema kuwa ripoti hiyo itaanza kufanyiwa kazi kuanzia sasa hadi Novemba ili kutoa maelekezo kwa hatua mbalimbali ambazo serikali itapaswa kuzichukua.Na Dodoma Fm
No comments:
Post a Comment